Ameingiliwa Kwa Nguvu Kiliwati, Je Ana Dhambi? Nini Hukmu Ya Liwati?

SWALI:

 

Assalam alaykum warahmatullahi wabarakat ama baada ya salam nakutakieni ramadhan maqbul. Kwa muislam alielawitiwa kwa kutezwa nguvu ni kweli hatoonana na MTUME (SAW). Na jee ni ipi hukumu yake.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kufupisha kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu kulawitiwa kwa nguvu.

Hakika ni kuwa si kweli kuwa mwenye kutenzwa kwa nguvu kufanya liwati au dhambi jingine lolote kuwa hatopata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amesema yafuatayo kuhusu kutenzwa nguvu:

 

Anayemkataa Allaah baada ya kuamini kwake - isipokuwa aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani” (16: 106).

 

 

Ama Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa kalamu imenyanyuliwa kwa mtoto mpaka abaleghe, aliyelala mpaka aamke na aliyelazimishwa.

 

Kwa hivyo, aliyeliwatiwa kwa nguvu bila kutaka hatokuwa na makosa wala madhambi bali madhambi yatakuwa kwa aliyetenda hicho kitendo.

 

 

Kuhusu hokum ya uliwati pata maelezo katika viungo vifuatavyo:

 

 

08 Kuharamishwa Liwati

 

 

Mwenye Kufanya Maasi Ya Liwati Anaweza Kurudi Kwa Allah Kutubia?

 

Mume Wangu Ananitaka Njia Isiyo Ya Halali

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share