Mja Mzito Asome Surah Gani Ili Imsaidie Katika Kuzaa?

SWALI LA KWANZA:

 

 

 

 

Assalam alaykum warahamtu llahi wabarakatu.

 

Shukurani zote zinamstahi Allah, Muumba wa kila kitu mbinguni na ardhini.

 

Ndugu zangu katika Uislam napenda kuuliza suala langu kama ifuatavyo. Kuna sura gani ambazo Mama Mjamzito anatakiwa kusoma kipindi chote cha ujauzito wake. Niliwahi kuambiwa kuwa unapokuwa mjamzito unatakiwa kusoma Surat- Maryam kila siku ili kupata afuwa katika hali yake hiyo.Naomba kupatiwa  ufafanuzi.

wabillahi taufiq

 

 

SWALI LA PILI:

 

Assalamu'alaikum Warahmatullahi Wabarakatuhuu.

 

Kwanza nachukua nafasi hii kwa kuwapongeza kwa kazi nzuri, mnayofanya ya kuelimisha jamii ya kiislam,mwenyezi mungu atawapa fungu lenu  insha’Allah.  

 

Swali langu ni : nina mdogo wangu anatarajia kujifungua mwezi huu   insha’Allah, sasa je kuna sura yeyote ile ambayo ataweza kusoma pindi uchungu utakapomuanza ili ajifungue kwa salama salmini?na je kama akiwa hawezi kuisoma, kutokana na uchungu je mumewe anaweza kumsomea?

 

wabillah tawfiq

 


 

 

JIBU

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakuna Surah maalumu ya kusoma kipindi mwanamke yuko katika uja uzito, bali anaweza kusoma Qur-aan Surah yoyote ile.

 

Wanawake wengi wana itikadi kwamba mja mzito asome Surah Maryam kwa vile imetaja uja uzito wa Maryam (‘alayhas-salaam) na kuzaa kwake.  Hakuna ushahidi kwamba wa jambo hilo, hivyo inabaki kuwa ni jambo la kuzushwa na haipasi kuweka itikadi hiyo.

 

Maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho:

 

 

Yanayopasa Kufanywa Na Mwenye Mimba Na Baada Ya Kuzaa

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share