Mume Kupokea Maiti Ya Mkewe Kaburini Akiwa Ametoka Kwenye Kitendo Cha Ndoa Kabla Ya Kufariki Mkewe

 

Mume Kupokea Maiti Ya Mkewe Kaburini Akiwa Ametoka Kwenye Kitendo Cha Ndoa Kabla Ya Kufariki Mkewe

 

Alhidaaya.com

 

Swali:

 

Asalam Alaykum warahmatulah swali langu linahusu kupokea mayti ndani ya kaburi je mume aliyefiwa na mke anaruhusiwa kupokea maiti hiyo iwapo alishiriki tendo la ndoa na mkewe muda mfupi kabla ya kufa kwa mkewe?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwa hakika jambo hilo limekatazwa kama zinavyoonyesha Ahaadiyth zifuatazo:

 

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kuwa, "Tulikuwa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati bint yake anazikwa. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anavujwa na machozi yakimiminika kwenye mashavu yake na akauliza, "Je, kuna kati yenu aliyefanya kitendo cha ndoa na mkewe usiku? Abu Twalhah akajibu, “Mimi sikufanya Ee Mjumbe wa Allaah.” Kisha Nabiy ((Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuamrisha ashuke ndani ya kaburi lake (la binti yake Nabiy) na kumzika." [Al-Bukhaariy].

 

Naye Imaam Ahmad katika riwaya nyingine kasimulia wka maneno yaliyo tofauti kidogo hivi: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: "Mtu aliyefanya tendo la ndoa na mkewe, hapaswi kuingia kwenye kaburi lake."

 

‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hakuingia kwenye kaburi la mkewe.

 

Kwa hiyo wataingia wale Mahaarim wake au watu wowote wengine.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share