Mke Ana Haki Kujua Mumewe Aendako?

SWALI:

 

ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATU-LLAHI WABARAKATU

 

MUME WANGU HUFANYA KAZI USKU, NA MCHANA WAKATI MWENGINE HUTOKA NA KWENDA KUTEMBELEA RAFIKI ZAKE, SHIDA HUJA WAKATI NNAPO MUULIZA MAHALI ANAPOKWENDA NAYE HUNIJIBU KWANI NILAZIMA NIMUUELEZE KILA MAHALI ANAPOKENDA NA KUWA RAFIKI ZAKE WOTE HUWA HAWA WAELEZI WAKE ZAO PAHALA WANAPO KWENDA, HATA MWISHO HUNIAMBIA IWAPO BABA YANGU HUMWAGA RUHUSA MAMANGU MARA KWA MARA ANAPOTAKA KUTOKA? JEE HII NISAWA MUME KUTOKA BILA KUMUARIFU MKEWE MAHALI ANAPO KWENDA AMA HANA HAKI KUJUA KITU? NINGEPENDA MUNIJIBU KWANI HUWA NAHUZUNI KWA MAJIBU KAMA HAYO KUTOKA KWA MUME WANGU.

MWENYEEZI MUNGU AWABARIKI.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu mke kumuuliza mumewe anapokwenda.

 

Ni vyema mume na mke (wanandoa) kuweza kuaminiana katika mambo yao. Kwa kufanya hilo ndio mapenzi hupatikana baina ya wanandoa, kunawiri na kushamiri.

 

Katika mambo ambayo yanaoleta mapenzi ni kwa mume kumuelezea mkewe hata bila ya kuulizwa kuwa mimi naenda mahali fulani na nitarudi saa kadhaa. Hilo litaleta kuaminiana kwa kiasi kikubwa baina ya wanandoa. Na pia linasaidia sana kujua alipo mumewe endapo kutatokeo jambo lolote lile. Na ni ada njema ambayo wanaume wanatakia waifuate ili kukuza mapenzi na maelewano. Ikiwa mume anakuwa mkali haina haja ya kugombana naye kuhusu hilo mwachilie tu bila kumuuliza.

 

Hakika hii ni haki ya pande zote mbili wanaume lakini wanaume kwa madaraka waliyopewa na sheria wanaona kuwa hawafai kuulizwa. Na kufanya hivyo si sawa kabisa kwa upande wao nah ali sivyo kisheria.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share