Kukidhi Swalaah: Swalaah Zinampita Anakuwa Njiani, Je Inabidi Akidhi Kila Siku Au Afanyeje?

 

Assalamu Aleikum,

 

Nafurahi kuijua hii website yenu na swali langu ni kuwa najua kama swala lazima iswaliwe kwa wakati wake. Lakini kama mimi mara nyingi natoka kazini saa sita na nafika nyumbani saa kumi unusu kwa sababu ya jam ya Nairobi. Pili pia saa ingine nawahi asri kazini natoka five lakini na fika kwangu saa mbili unusu niko njiani sasa nifanyeje nisizilipe au vipi. Tafadhali nielimisheni.

 

Shukran


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kukutwa na msongamano wa magari barabarani hadi kushindwa kuswali Swalah kwa wakati wake.

Mwanzo tufahamu kuwa Swalah ikipita wakati wake ni lazima uilipe wala huo hautakuwa ni udhuru wako wewe kuacha kuswali. Kuacha kuswali ni ukafiri.

 

Hatujui ndugu unafanya kazi wapi Nairobi na unaishi wapi. Kutoka kazini saa sita na kufika saa kumi na unusu ni muhali ila tu uwe unafanya nje ya Nairobi hivyo kulazimika pengine kutumia usafiri wa umma aina ya ‘matatu’ mbili ili kufika nyumbani. Ikiwa unatoka wakati huo unaweza kuchelewa kuondoka pale kazini ili uswali Swalah ya Adhuhuri na kuswali Swalah ya Alasiri unapofika nyumbani. Na ikiwa siku utatoka saa kumi na moja, hakikisha unapochukua wudhuu wako wakati unakwenda kungojea matatu. Pindi unapofika wakati unaweza kuswali ndani ya gari na huku umekaa na kufanya hivyo utasalimika na balaa ya kutoswali kwa wakati.

 

Ama ikiwa una usafiri wako binafsi unaendesha, basi jitahidi upitie sehemu ambayo kuna Msikiti au sehemu unayoweza kutekeleza ‘Ibaadah yako kabla haijakupita.

 

Tuaamini ikiwa utatumia njia hii basi hutokuwa na matata wala tashwishi ya aina yoyote ile.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share