Mwezi Kuonekana Baina Ya Nyota Mbili Zilokuwa Ziking’ara Ni Ishara Gani?

 

Mwezi Kuonekana Baina Ya Nyota Mbili Zilokuwa Ziking’ara Ni Ishara Gani?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

A.Alykum nimefurahishwa sana na website yenu na Inshallah kutoka saiv nitakuwa najiunga na nitakuwa mwanachama ktk website ALLAAH aizidishie wepesi zaidi. Suala langu:  Hivi karibuni niliona mwezi upo katikati baina ya nyota mbili nyota hizo zilikuwa zkingara cna mpaka zikanitia hofu pamoja na mwezi wake uking'ara. Ningeliomba kufham kma kuna maana yyte mwezi kuwa katikati ya nyota mbili na kungara kuliko kawaida yke.Kwa sababu cku ya pili nilipoangalia ckuona mwezi kungara cna wala haukuwa ktkt ya nyota zile ambazo mara nyingi huwa karibu na mwezi sijawahi kuziona kukaa katikati zaid ya siku hiyo moja.WABILLAH TWAFIQ

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Kwanza kabisa tunapenda kuwakumbusha wote wenye kuzoea kufupisha Salaam au kufupisha kumswalia Nabiy wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ni bora waache kufanya hivyo na waandike kwa urefu kwani zote hizo ni 'Ibaadah na ni bora kuzifanya kwa ukamilifu ikiwemo katika kuandika, kutamka n.k. Pia kuongeza neno 'Ta'aalaa' kwenye Salaam kwa kusema 'Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaahi Ta'aalaa wa Barakaatuh', si jambo tulilofundishwa katika Salaam na hivyo ni bora mtu kuliepuka katika Salaam.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwezi kuonekana baina ya nyota mbili.

 

Jambo hili mbali na kuwa linaonekana kuwa kinyume na maumbile kwani katika enzi zetu hatujawahi kuona hilo. Hata hivyo, huenda kwa sababu ya kutotaamali kwetu likawa limetokea hata zaidi ya hilo.

 

Tufahamu kuwa hakuna maajabu yoyote kwa hilo kufanyika kwani nyota na mwezi ni miongoni mwa viumbe vya Allaah Aliyetukuka. Na jambo lililokuwa si la kawaida lilitokea wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akaondoa itikadi ambazo zilikuwa zinataka kujitokeza ambazo hazikuwa nzuri.

 

 

"Mtoto wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiitwa Ibraahiym aliaga dunia siku ambayo jua lilipatwa. Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wakaanza kusema kuwa jua limepatwa kwa ajili ya kifo cha Ibraahiym. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawarekebisha Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) kwa kuwaambia kuwa jua ni kiumbe kama viumbe vyengine vya Allaah Aliyetukuka, havipatwi kwa kufa au kuzaliwa kwa yeyote yule".

 

Kwa hiyo, mwezi kuonekana katika hali hiyo na nyota mbili ni miongoni mwa ishara Zake Aliyetukuka haina maana yoyote nyingine. Tayari zipo ishara nyingi sana zinazotufahamisha kuwepo Yeye Aliyetukuka na uwezo Wake.

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share