Imaam Asiyesoma Vizuri Qur-aan Anafaa Kuswalisha?

SWALI:

 

Assalamu Alaykum,

 

Imamu ambaye hasomi vizuri Qur-an kiasi ambacho hawezi kusalisha Swala za Jahra (Magharibi, Isha na Asubhi), jee anaweza kutusalisha katika Swala za siri kama vile Adhuhuri na Alasiri?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Imaam asiyesoma vizuri Qur-aan katika Swalah.

 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuusia kuwa Imaam anatakiwa awe ni mjuzi juu ya wengine kwa kisomo cha Qur-aan. Ikiwa wapo wawili walio sawa kwa ujuzi na elimu ya somo hilo, basi atazamwe aliye mjuzi wa Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na ikiwa kwa kipengele hicho pia wapo sawa basi atatizamwa yule ambaye ni mkubwa zaidi kwa umri awe Imaam.

 

Ikiwa Imaam ni hivyo ulivyosema itabidi mjaribu kutazama aliye mzuri zaidi au ikiwa amechaguliwa na wasimamizi wa Msikiti basi mzungumze na wasimamizi wa Msikiti ili aangaliwe mwengine wa kuongoza Swalah. Na lau atakuwa hasomi vizuri Qur-aan lakini yeye ndiye bora katika mtaa au eneo hilo, basi huyo ndiye atakayeendelea kuwa Imaam hadi apatikane mwengine.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share