Uyoga (Mushroom) Wa Sosi Na Jibini

Vipimo
Uyoga 12 au zaidi
Siagi 2 vijiko vya supu
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) 1
Nyanya ilosagwa 3 vijiko vya supu
Kitunguu thomu kilosagwa 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga ½ kijiko cha chai
Oregano 1 kijiko cha chai
Parsely kavu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Nanaa kavu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Jibini (cheese) ya mazorella* 250 gm
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha uyoga vizuri, kisha weka siagi katika sufuria ishike moto. Tia uyoga ukaange kaange kidogo ili ulainike uyoga.
- Katika kisufuria kidogo, weka mafuta, kaanga kitunguu hadi vigeuke rangi.
- Tia thomu, kaanga zaidi kidogo, kisha tia nyanya na bizari zote kaanga tena kidogo.
- Panga uyoga katika treya ya kupikia katika oveni, kisha mwagia sosi juu yake.
- Kuna jibini ya mazorela umwagie juu yake pia.
- Pika (Bake) katika oveni moto wa kiasi hadi uyoga upikike zaidi na jibini iyayuke. Epua ukiwa tayari.
Kidokezo :
Ikiwa idadi ya uyoga ni kidogo, basi sosi itakayobakia unaweza kutumia katika Pizza au pasta.
* unaweza kutumia aina nyengine ya jibini
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
