Mbaazi 2

Vipimo
Mbaazi za kopo 2
Kitunguu 1
Chumvi kiasi
Manjano ½ kijiko cha chai
Kidonge cha supu kipande kidogo
Mafuta 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi 2 nzima
Nazi 3 ½ vikombe
Namna Ya Kutayarisha Nkupika
1. Osha mbaazi kwenye chungio na ziache zitoke maji.
2. Kaanga kitunguu kidogo tu kisha tia mbaazi na majano.
3. Tia kidonge cha supu na chumvi pilipili mbichi na nazi
vikombe vitatu, utabakisha nusu kikombe.
4. Ikisha kauka kidogo changanya nazi ya unga
vijiko 4 vya supu kwenye nazi uliobakisha, mimina kwenye mbaazi.
5. Iache motoni kidogo hadi iwe nzito na itakuwa tayari kuliwa kwa maandazi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
