Kusafisa Mafigo (Kidney Dialysis) Inabatilisha Swawm?

SWALI:

 

ASSALAMA ALAYKUM WA RAHMATU LLAHI TAALA WA BARAKATU REHMA NA BARAKA ZA MOLA WETU MTUKUFU ZIWAFIKIE POPOTE PALE MLIPO AMEEN

 

SHEKH MM NAPENDA KUWAULIZIA WALE NDUGU ZETU WALIO PATA MARADHI YA FIGO NA AMBAO WANASAFISHA MAFIGO KWA WIKI MARA TATU AU HATTA MARA MOJA JEE VIPI FUNGA YAO INAKUBALIKA. JAZAKUMU LLAHI KHER NAOMBA KUJIBUWA KWA HARAKA SABABU WAGONJWA WANASUBIRI JAWABU NA TUNAWASHUKURU SANA KATIKA JUHUDI ZENU MNAZO ZICHUKUA KATIKA MASALA YA DINI YETU YA ISLAAM 

 

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kuhusu wagonjwa wenye  kuhitaji kusafishwa  mafigo (kidney dialysis) ni kwamba Halmashauri (Jopo) Ya Kudumu Ya Utafiti Wa Kiislaam imetowa Fatwa kwamba kusafisha mafigo (kidney dialysis) inabatilisha (inavunja) Swawm.  Hivyo basi mwenye ugonjwa huo, hapasi kufunga siku anazofanya usafishaji huo wa figo. Akiweza atalipa siku hizo baada ya Ramadhaan, na ikiwa hawezi kulipa kutokana na hali ya afya yake, basi  alishe maskini mmoja kila siku.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo kuhusu kafara ya Swawm:

 

 

Kulipa Swawm Na Kafara

  

Hakuweza Kufunga Kwa Muda Wa Miaka Minne Kwa Sababu Ya Ugonjwa

 

Mwenye Deni La Swawm Ikiwa Ana Ugonjwa Wa Kuhitaji Kutumia Dawa Kwa Wakati Bila Kuacha, Afanyeje?

 

Fidia Asiyeweza Kufunga Anaweza Kulipa Baada ya Ramadhaan?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi  

 

 

Share