Anataka kuunganisha Swalah Kwa Khofu Ya Kuweko Najasa Ya Mbwa

SWALI:

 

Assalam alaikum,

 

I have a question about prayers. I am living in Netherlands. Since it’s a Christian country praying inside our office is kind of hard, because there are dogs coming inside and they lick you. But I heard that I can pray my Dhuhr and Asr prayer in the morning. Is it allowed? I talked to one of my family member that he is also living here and he said I should ask by Alhidaaya. Thank you,

                              


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuunganisha Swalah kwa ajili ya hofu ya najasa.

Mwanzo inafaa tuelewe Muislamu hawezi kuswali kabla ya wakati wake kuingia, kwani kuingia wakati ni sharti katika kutimia Swalah. Kwa ajili hiyo lau mtu ataswali kabla ya kuingia wakati kama vile kusema kuswali asubuhi Swalah za adh-Dhuhr na al-‘Aswr ni jambo ambalo halikubaliki kishari’ah. Kuhusu umuhimu wa kuswali kwa wakati wake Allaah Aliyetukuka Amesema:

Hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu” (an-Nisaa’ [4]: 103). Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza sana Waislamu waswali Swalah tano kwa wakati wake makhsusi uliowekwa.

 

Kisha kuunganisha Swalah kuna masharti yake na njia zake, na kuwa na najisi si miongoni mwa sababu za watu kuunganisha Swalah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kuwa ardhi yote ni Msikiti na twahara. Sisi ndio tunajitia katika mashaka.

Ikiwa hapo ndipo pekee mnaweza kuswali mnaweza kutafuta karatasi za kuweka juu yake au mikeka au miswala na wakati wa Swalah ukifika mkaswali. Au mnaweza mkatafuta sehemu nyingine kwenye uwanja, nyasi nje, maadamu najisi haionekani unaweza kuswali tu sehemu hiyo. Ama kunuswa na mbwa mnatakiwa mtahadhari, kwani wanyama wenyewe wana maradhi kwa yale maji maji yao.

 

Njia nyingine ni nyinyi kuzungumza na idara ya sehemu mnayofanya kazi ili wawadhibiti hao mbwa wasiwe ni wenye kuingia. Ni ajabu kwa nchi hizo zinazosema zimeendelea kuacha mbwa kuzurura ovyo hata katika maofisi. Inatakiwa mfanye bidii kuhusu ‘Ibaadah muhimu kama Swalah kuiswali kwa wakati wake na bila shaka Allaah Aliyetukuka Atawasaidia.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share