Mtoto Wa Kiume Aliyebaleghe Anafaa Kumuosha Baba Yake?

 

Mtoto Wa Kiume Aliyebaleghe Anafaa Kumuosha Baba Yake?

 

Alhidaaya.com

 

Swali:

 

Asalam Aleykum,

 

Nauliza – Mtoto Aliyebaleghe Wa Kiume Anaruhusiwa Kumuosha Baba Yake.

 

 

Jibu: 

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakika ni kuwa ni muhimu zaidi katika kuosha mtu aliyeyekufa awe ni jamaa ya maiti wa karibu. Na ikiwa mtoto yupo basi ni bora zaidi kwani yeye hasa akimuosha mzazi ataweza kuficha aibu ya mzazi wako.

 

Kitu muhimu ambacho kinahitajika kwa huyo mtoto kuweza kuosha mwili wa babake ni kuwa na elimu pamoja na ujuzi wa kufanya kazi hiyo. Ikiwa atakuwa na masharti hayo basi ataruhusiwa na shari’ah bila ya wasiwasi wowote ule.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share