Akisahau Kusoma Du'aa Ya Qunuut Je, Afanyeje?

SWALI:

 

Assalaam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh baada ya maamkizi hayo mema shukran zangu ziende kwa Mola wetu aliyetuumba Subhaana wa Ta‘ala na pia alhidaaya. Sheikh nina maswali mengi kuhusu swala itakuwa vizuri kama utapata muda kunielimisha.

 

KWANZA-Dua ya Qunut ktk swala ya fajri ni vizuri kuisoma lkn kama utasahau basi haina tatizo, Je ktk swala ya witri ni lazima au ukisahau urudie raka.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu du’aa ya Qunuut katika Swalaah ya Witri. Du’aa ya Qunuut ni vyema kuileta katika Swalah ya Witr lakini ikiwa utasahau hutorudia rakaa na Swalaah yako ni sawa kabisa. Tufahamu kuwa Qunuut si katika nguzo wala wajibu wa Swalah.

Ama Qunuut katika Swalah ya Alfajiri si sahihi kusema kuwa ni vizuri kuisoma, bali ilivyo ni kuwa haijathibiti kwa ufahamu sahihi wa Hadiyth sahihi kuwa kulikuwa na Qunuut kwa Swalah ya Alfajiri tu! Hivyo, Qunuut katika Swalah ya Alfajiri haipo na ni vizuri kutoitekeleza, lakini ikiwa umefika Msikitini na kwenye Msikiti huo kunasomwa Qunuut ya Alfajiri, basi unaweza kuswali na wala usiache kuswali kwa sababu wanasoma Qunuut Alfajiri.

Soma zaidi kuhusu Qunuut:

Kusoma Du'aa Ya Qunuut Katika Swalah Ya Alfajiri Ni Sunnah?

Du'aa za Qunut Ziko Ngapi Na Je Lazima Zisomwe Katika Swalah Ya Alfajiri?

Anamkhalif Imaam Kwa Kusoma Du'aa Ya Qunuut Wakati Imaam Anasujudu

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share