Ndoa Bila Wazazi Wala Mashahidi

SWALI:

 

Baada ya salam hiyo ningependa kuuliza swali zangu kadhaa Mwanamke kukubaliana na mpenzi wake kua mk na mume nakuelewana kabisa mahali pasi na mashahidi au wazazi kujua hiyo inaweza kua ndoa tosha natiari kukutana kimwili??


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ndoa bila ya idhini ya wazazi wala mashahidi. Hakika suala hilo limejibiwa na yeye mwenyewe, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema: “Hakuna ndoa bila ya idhini ya walii wala mashahidi wawili waadilifu”. Kwa hiyo haya masharti mawili pamoja na mengineo ni muhimu kusihi ndoa ya Kiislamu. Masharti katika Hadiyth iliyo juu ni:

 

1.       Idhini ya walii (baba akiwepo na akiwa hayuko basi wale walio karibu na mwanamke kwa upande wa baba).

 

 

2.       Kuwepo kwa mashahidi wawili walio waadilifu.

 

Kukosekana kwa masharti hayo yaliyo juu ni kuwa ndoa ya hao wawili haikusihi na ikiwa watakuwa wanaishi pamoja watakuwa wanazini wala kishari’ah hawatochukuliwa kuwa ni wanandoa.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:

 

 

Ndoa Ya Siri Inafaa Ikiwa Wazazi Hawataki?

 

Ndoa Ya Siri Inafaa?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share