Sunni Anaweza Kuolewa Na Shia?

 

 

SWALI:

 

Asalam aleykum! Labda nitakua nimekosea mniweeradhi. Mimi nina maswali; je Sunni anaweza kuolewa na Shia?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Awali ya yote hakuna haja kabisa ya kuomba msamaha kwa swali unalouliza kwani hiyo ni haki yako.

 

Pili, hakuna uwezekano wa Msuni kuolewa na Mshia kwa sababu itikadi za hawa wawili zimetofautiana katika misingi ya Dini kwa kiasi kikubwa. Mshia ni mtu ambaye anawatusi Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na kuwachafua wake za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kwenda hata kinyume na Qur-aan inayowasifu kwa sifa nzuri kabisa, pamoja na itikadi zao za kishirikina na kufru zilizojaa kwenye vitabu vyao vya kuaminika kama Al-Kaafiy na vinginevyo.

 

Ukweli Juu Ya Al-Kaafiy (Kitabu Cha Hadiyth Cha Kutegemewa Cha Mashia)

 

 

Kadhaalika, Imaam wakubwa za kale na wa sasa wamepinga jambo hilo kwa nguvu na kwa hoja mbalimbali, na hata kufikia kusema Suni mwanamme vilevile haipendezi kumuoa mwanamke wa kishia.

 

Soma maelezo ya Imaam wakubwa kuhusiana na Mashia:

 

Maoni Ya Maimaam Kuhusu Mashia

 

Vilevile bonyeza kiungo kifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu upotofu wa ‘Aqiydah za Mashia:

 

Itikadi Potofu

 

Itikadi Potofu Za “Shia” Kama Ilivyoandikwa Kwenye Vitabu Vyao - 1

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share