Kuswali Rakaa Mbili Za Wudhuu Japokuwa Wakati Wa Makruuh Inafaa?

SWALI:

 

Jee mtu aweza kusali raka mbili killa anapo tawadha  kama alivyokuwa akifanya Bilal Radhiya  Allahu anhu wakati wa makrooh kusali baada ya salat Alfajr mpaka shurook na baada ya salat Asr lakini ikiwa ni kawaida yako kusali killa unapotawadha na udhu ukakutoka baada ya hizo sala na ukachukua udhu jee usali rakaa mbili au haifai?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kuswali rakaa mbili baada ya kuchukua wudhuu.

 

Hakika ni kuwa katika suala la Swalaah ambazo ni za Sunnah kuna zile ambazo zina sababu makhsusi na nyingine ambazo zimesuniwa kabla au baada ya faradhi.

 

Ama zile ambazo ni kwa sababu maalumu kama Sunnah ya wudhuu au ya Tahiyyatul Masjid hizo zinaweza kuswaliwa wakati wowote ima baada ya kuchukua wudhuu au kuingia Msikitini.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share