Hadiyth Kuhusu Kuteremka Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) Na Kuwa Amiri Wa Waislamu Ni Sahihi?

SWALI:

 

Assalaam Aleykum Warahmatullahi. Jee Vipi Katika Hadiysi Hii Mapokezi Yake Yapo Sawa Hapa?


Hakutakosekana kuwa na kikundi katika Ummah wangu, wakipigana juu ya haki wakiwa washindi haki Siku ya Qiyaama… kisha 'Iysa bin Maryam atashuka, na Amiri wao (Waislamu) atasema: 'Njoo utuswalishe katika Swalah!' Atasema: 'Hapana, nyinyi ndio ma-Amiri juu ya kila mmoja kama heshima kutoka kwa Allaah kwa Ummah huu'" (Muslim).

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu usahihi wa Hadiyth uliyoitaja hao juu kuhusiana na ‘Iysaa bin Maryam (‘Alayhis Salaam).

Kama ulivyoashiria kuwa Hadiyth hiyo iko katika Swahiyh Muslim na imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhiya Allaahu ‘anhuma). Hadiyth hiyo ni sahihi kabisa na haina shaka yoyote ile.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share