Anaweza Kumfanyia Mzazi Aliyefariki Hajj?

 

 

Anaweza Kumfanyia Mzazi Aliyefariki Hajj?

 

 Alhidaaya.com

 

 

Swali:

  

Aww, ninaulizo kuhusu hija, sheriya inakubali mtoto kumfanyiya hija mzazi wake kama alifariki?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwanza tunakukumbusha ndugu muulizaji, kutokufupisha salaam unaposalimia. Iandike kikamilifu upate ujira kamili In shaa Allaah.

 

Tukirudi kwenye swali, Shari’ah hakika inaruhusu mtoto (kijana) kumfanyia Hijjah mzazi na Hijjah hiyo itahesabiwa ni ya mzazi. Hata hivyo, inatakiwa awe mtoto mwenyewe ashafanya Hijjah. Mtoto hawezi kumhijia mzazi ikiwa yeye mwenyewe hajahiji.

 

Mtoto akishahiji na akawa na uwezo wa kumfanyia mzazi wake Hijjah itakuwa vyema.

 

Zaidi pia unaweza kusoma katika viungo vifuatavyo:

 

Kumhijia asiyehiji

 

Kumgharimia Mtu Hijjah Kabla Ya Kufanya Mwenyewe Inafaa?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share