Anaweza Kuingia Msikitini Na Kifuko Cha Mkojo Kutokana Ugonjwa?

 

Anaweza Kuingia Msikitini Na Kifuko Cha Mkojo Kutokana Ugonjwa?

 

 

 

SWALI:

 

SALAAM ALEIKUM WARAHMATU ALLAH WABARAKAT NDUGU SUALI LANGU YUKO RAFIKI YANGU MGONJWA AMEFANYIWA OPERATION KATOLEWA KIBOFU CHA MKOJO NA HIVI SASA ANATUMIA MFUKO WA KUHIFADHI MKOJO UKIJAA ANAKENDA CHOONI KUUMWAGA ANAULIZA VIPI INAJUZU KUINGIA MSIKITINI NA MFUKO WA MKOJO? ASANTE SANA NASUBIRI JAWABU

 

 

JIBU:

 

 AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Uislamu ni Dini ambayo inamtakia mwana Aadam sahali na wepesi mkubwa sana. Uislamu hautaki kumtia mtu katika jambo ambalo litakuwa ni vigumu kwake kutekeleza. Kwa minajili hiyo, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Anasema:

 

 

Ndiye Amekuteueni na Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika  [Al-Hajj: 78]

 

Na Anasema pia:

 

Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake [al-Baqarah: 286]

 

Hivyo, ikiwa kuna taklifu yoyote ile mgonjwa anaweza kuswali nyumbani kutokana na dharura kama hizo. Lakini ikiwa ataona kwamba hakutakuwa na taklifu yoyote wala uzito wowote ule basi mgonjwa huyo anaweza kwenda Msikitini na hiyo ni bora zaidi na fadhila zaidi, bora tu ahakikishe amekisafisha kabla ya Swalaah, na kuwa mkojo hautovuja au kumwagika na kuingia kwenye sehemu ya kuswalia. Ikiwa hali itakuwa hivyo, basi kutakuwa hakuna tatizo kwani kifuko kiko ndani ya nguo, kimesitirika barabara na hakuna harufu inayotoka nje.

 

Mara nyingi kwa wagonjwa wa aina hiyo huwa wanashauriwa kwa muda wasiwe ni wenye kwenda mbali mpaka baada ya muda. Ni bora na vyema akae nyumbani mpaka akatakapotulia ili mwendo huo usije ukampatia taklifu ya bure.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share