Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) 4-Kuharamishwa Kwake Na Adhabu Zake Katika Quraan
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((وَلاَ تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْؤُولاً))
((Wala usifuate (ukipita ukisema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo hivyo vyote vitaulizwa)) [Al-Israa: 36]
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
(( وَلاَ يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ))
((Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia
Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameharamisha Muumimi kumsengenya mwenziwe
Maulamaa wamekubaliana kuwa Ghiybah ni haraam
Kauli:
(( فَكَرِهْتُمُوهُ ))
((Mnalichukia
kwa maana
Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((وَلاَ تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الاِسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ))
((Wala msitukanane kwa kabila wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasiotubu, hao ndio wenye kudhulumu)) [Al-Hujuraat: 11]
Mwenye kufanya hivyo; mwenye kusengenya na mwenye kumzushia mwenziwe uongo wamelaaniwa na kushutumiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Aayah ifuatayo:
((وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ))
((Ole wake kila safihi, msengenyaji!)) [Al-Humazah: 1]
Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Humazah ina maana yule anayetukana na kufedhehesha wenziwe" [At-Twabariy 24: 596]
Al-Hammaaz: Mwenye kusengenya kwa vitendo kwa mkono au kwa macho
Al-Lammaaz: Mwenye kusengenya kwa ulimi (kunena).
[Kauli ya Mujaahid katika Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]
Yote hayo ni Ghiybah na adhabu zake ni
1. Neno la kutisha lenye maana ya kudhalilishwa, kuadhibiwa na kungamizwa.
2. Ni bonde katika moto wa Jahannam
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa wanaosengenya kwa kuzulia watu maovu,
((إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ))
((Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu iumizayo katika dunia na Akhera. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui)) [An-Nuur: 19].
************
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
