Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) 5-Kuharamisihwa Kwake Na Na Adhabu Zake Katika Sunnah
عن أبي بكرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال في خطبته يوم النحر بمنى في حجة الوداع: (( إن دمائكم، واموالكم وأعراضكم حرام عليكم كحرمة يومكم هذا، في شهركم هذا، في بلدكم هذا، ألا بلغت )) متفق عليه
Kutoka kwa Abu Bakrah (Radhiya Allaahu 'anhu) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika khutba yake ya siku ya An-Nahr [siku ya kuchinja – yaani siku ya 'Iydul-Adhwhaa] huko Minaa katika Hajjatulwadaa' [Hijjah ya kuaga] ((Hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni haramu kwenu kama uharamu (wa kutenda dhambi) siku yenu hii katika mji wenu huu. Je nimefikisha?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth hii inatuonyesha jinsi gani makatazo hayo yaliyotajwa, yakiwemo ya kuvunjiana heshima yalivyokuwa mazito kwamba ni sawa na kutenda dhambi mji mtukufu na siku tukufu hiyo ya Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja). Bila ya shaka kila mmoja wetu atapima umuhimu huu wa kuhifadhi heshima za wenzetu kwa kutowasengenya na kutoa aibu zao kwa wengine.
Ikiwa hata mtu ana sifa ambayo unaitaja nyuma yake huwa in maana ni kumsengenya
عن عائشة رضي الله عنها قالت: قلت للنبي صلى الله عليه وسلم حسبك من صفيه كذا وكذا. وقال بعض الرواة: تعني قصيرة، فقال: (( لقد قلت كلمة لو مزجت بماء البحر لمزجته )) قالت: وحكيت له إنسانا فقال: (( ما احب أني حكيت إنسانا وان لي كذا وكذا )) رواه أبو داود والترمذي وقال: حديث حسن صحيح.
Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesimulia: "Nilimwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Achana na Swafiyyah; yuko kadhaa na kadhaa" yaani ni mfupi – Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika umetamka neno ambalo lau lingalichanganywa na maji ya bahari yangelibadilika)) (kutokana na uvundo wa neno
Dini yetu ya Kiislam imesisitiza
عن عبد اللَّه بن عَمْرو بن الْعاص رضي اللَّه عنهما عن النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : ((الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسانِهِ ويَدِهِ ، والْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ ما نَهَى اللَّه عَنْهُ)) متفق عليه
Kutoka kwa 'Abdullaahi bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislam ni yule wanaosalimika Waislam kwa ulimi wake na mkono wake, na Muhaajir (mwenye kuhama) ni yule anayehama yale Aliyoyakataza Allaah )) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Umuhimu wa kuhifadhi ulimi ili usimuingize mtu motoni:
عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ))
.ثم قال: (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: ((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ)) - حتى بلغ – ((يَعْمَلُونَ)) السجدة: 16-17 .
ثم قال: ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).ثم قال: ((ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) . قلت: يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ, وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ )) أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ ألسِنَتهم)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allaah! Niambie kitendo ambacho kitanipeleka peponi na kitaniokoa na moto. Akasema: ((Umeniuliza jambo kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambaye Mola Amemsahilishia. Muabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zakaah, funga Ramadhaan, nenda kuhiji (Makka). Kisha akasema: ((Je? Nikuonyeshe milango ya kheri? Swawm ni ngao, Sadaka inazima dhambi
Tena akasema: ((Je, nikwambie kilele cha
Baadhi ya hizo adhabu za Akhera alikwishaziona Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokwenda Israa wal Mi'raaj na katuelezea katika Hadiyth ifuatayo:
عن أنس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( لما عرج بي مررت بقوم لهم أظفار من نحاس يخمشون وجوههم وصدورهم، فقلت: من هؤلاء يا جبريل؟)) قال: هؤلاء الذين يأكلون لحوم الناس ويقعون في أعراضهم"
Kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nilipopandishwa mbinguni (Siku ya Israa na Mi’raaj) nilipita kwa watu ambao walikuwa wana kucha za
************
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
