Tafauti Kati Ya Aayah Zilizokuwa Zikishuka Makkah Na Zilozoshuka Madiynah

 

Tafauti Katika Ya Aayah Zilizokuwa Zikishuka

Makkah na Zilizoshuka Madiynah

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleykum.kila Sifa Njema Anastahiki Rabb Wa Viumbe Vyote Allah Tabaraka Wataala. Naomba Kupata Ufafanuzi Wa Tofauti Kati Ya Aya Zilizokua Zikishuka Madinah Na Aya Zilizokua Zikishuka Makkah Zilikua Na Tofauti Gani.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Tofauti kubwa inayoonekana baina ya Aayah zilizoteremka sehemu hizo mbili tofauti ni:

 

1.  Aayah za Suwrah za Makkah ni za kujenga Imani na umuhimu wake Makkah lakini Madiynah ikawa ni shari’ah na utendaji kazi wake.

 

2.   Visa vya Ummah iliyopita katika Aayah za Makkah ilhali Aayah za Madiynah ni kuhusiana na ‘Ibaadah.

 

3.   Aayah na Suwrah za Makkah ni fupi ilhali za Madiynah zilikuwa ni ndefu.

 

4.  Kubainishwa halali na haramu katika kipindi cha Madiynah ilhali Makkah hakukuwa na Aayah aina hizo.

 

5.   Aayah kuhusiana na shirki na ukafiri huko Makkah ilhali Madiynah ni Aayah kuhusiana na waliopewa Kitabu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share