Mboga Mchanganyiko Na Sosi Ya Uyoga

Mboga Mchanganyiko Na Sosi Ya Uyoga 

  

Vipimo

Viazi - 2

Karoti - 2

Koliflawa (cauliflower) - ¼ ya uwa zima

Brokoli (brocoli) -1 mshikano mdogo (bunch)

Uyoga (mushrooms) -  12-13

Figili mwitu (celery) - 1 mche

Nanaa kavu (dry mint leaves) - 2 vijiko vya supu

Pilipili manga - ½ kijiko cha supu

Kidonge cha supu (stock) - 1

Chumvi - Kiasi

Siagi - 1 kijiko cha supu

Maziwa - 2 vikombe 

Namna Ya Kupika Mboga:    

  1. Changanya pamoja katika bakuli, viazi, karoti, koliflawa, brokoli, nusu uyoga, figili mwitu, koleza chumvi kidogo pilipili ukipenda.  
  2. Weka katika bakuli la kupikia ndani ya oven, funika  upike (bake) kwa moto wa kiasi hadi mboga ziive. Mboga ziive kiasi tu si mpaka zivurugike. 
  3. Epua weka kando utayarishe sosi ya uyoga.   

Namna Ya kupika Sosi Ya Uyoga 

  1. Weka nusu uyoga ulobaki katika mashine ya kusagia (Blender), tia maziwa, kidonge cha supu, pilipili manga, kisha piga ilainike.  
  2. Tia siagi katika kibakuli kidogo weka motoni, mimina sosi  uipike kidogo iwe nzito kidogo.  
  3. Changanya na nanaa kavu, pilipili manga kidogo tena, umwagie juu ya mboga uchangaye vizuri.

 

 

 

 

 

Share