018-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Alama Za Mnafiki Ni Tatu: Uongo, Kutokutimiza Ahadi, Kufanya Khiyana

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 18  

Alama Za Mnafiki Ni Tatu: Uongo, Kutokutimiza Ahadi, Kufanya Khiyana

www.alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((آيَةُ الْمُنَافِقِ ثلاَثٌ إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ)) متفق عليه . وفي رواية: ((وَإِنْ صَامَ وَصَلَّى وَزَعَمَ أَنَّهُ مُسْلِمٌ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Alama za mnafiki ni tatu: anapozungumza husema uongo, anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi), na anapoaminiwa hufanya khiyana)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na katika riwaaya nyingine: ((Hata akifunga na akiswali na akidai kuwa yeye ni Muislamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Unafiki ni miongoni mwa maradhi ya moyo yanayokemewa sana katika Uislamu. Rejea: Al-Maaidah (5: 52), Al-Anfaal (8: 49).

 

 

2. Sifa tatu hizo ni sifa mashuhuri miongoni mwa sifa za wanafiki. Rejea: An-Nisaa (4: 143), Al-Baqarah (2: 8-15) Lakini hizo sio sifa pekee zinazowahusu wanafiki, bali wanazo sifa mbaya zaidi ya hizo.

 

 

3. Mwenye kuwa na sifa zote tatu hizo atahadhari mno kwani ni sifa mbaya mno asizopasa kuwa nazo Muislamu!

 

 

4. Kukimbilia kujirekebisha pindi Muislamu anapotambua kuwa ana sifa mojawapo kabla ya kumiliki sifa zote tatu.

 

 

5. Uislamu unafunza sifa njema za ukweli, kutimiza ahadi na uaminifu. Rejea: An-Nisaa (4: 58), An-Nahl (16: 91). Na sifa hizo njema ni miongoni mwa sifa za watakaopata Jannah ya Al-Firdaws Rejea: Al-Muuminuwn (23: 8). Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ﴿٣٢﴾

Na ambao amana zao na ahadi zao ni wenye kuchunga (na kuzitimiza). [Al-Ma’aarij (70: 32)]

 

 

6. Mtu anaweza kuwa na mandhari nzuri kwa mavazi na matendo ya uswalihina lakini  huenda akawa ana sifa za unafiki kama hizo. Na hii ni hatari kwake kwani Allaah ('Azza wa Jalla) Hatazami mandhari wala sura bali Anatazama yaliyo moyoni mwake.

 

 

Rejea Hadiyth namba (89), (125).

 

Share