052-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Muumin Angelijua Adhabu Za Allaah Asingelitarajia Jannah, Kafiri Angelijua Rahma Ya Allaah Asingelikata Tamaa Nayo

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 52

Muumin Angelijua Adhabu Za Allaah Asingelitarajia Jannah,

Kafiri Angelijua Rahma Ya Allaah Asingelikata Tamaa Nayo

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَوْ يَعْلَمُ الْمُؤْمِنُ مَا عِنْدَ اللَّهِ مِنْ الْعُقُوبَةِ مَا طَمِعَ بِجَنَّتِهِ أَحَدٌ. وَلَوْ يَعْلَمُ الْكَافِرُ مَا عِنْدَ اللَّهِ مِنْ الرَّحْمَةِ مَا قَنَطَ مِنْ جَنَّتِهِ أَحَدٌ)) مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Lau Muumin angalijua adhabu zilioko kwa Allaah, hakuna yeyote angelitarajia kuingia katika Jannah Yake. Na Lau kafiri angalijua Rahma zilioko kwa Allaah, hakuna yeyote angekata tamaa ya Jannah Yake)). [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Kukhofia adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى) na kutaraji Rahma Zake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

Mwenye kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa kuakibu, Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Mwabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia. [Ghaafir (40: 3)

 

Rejea pia: Al-Maaidah (5: 98), Az-Zumar (39: 53).

 

 

2. Muumin anapaswa kuwa katika hali ya khofu na matarajio hata anapotenda mema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوا وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَىٰ رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ ﴿٦٠﴾

Na ambao wanatoa vile walivyopewa na huku nyoyo zao zinakhofu kwamba hakika watarejea kwa Rabb wao.

 

أُولَـٰئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ ﴿٦١﴾

Hao wanakimbilia katika mambo ya kheri; na wao ndio wenye kuyatanguliza.  [Al-Muuminuwn (23: 60-61)]

 

 

3. Muumin anatakiwa akimbilie kutenda mema apate Rahma na malipo mema ya Rabb wake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾

Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji rahmah ya Allaah, na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah (2: 218)]

 

 

4. Rahma ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni pana mno, na adhabu Yake ni kali mno. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

 (Allaah) Akasema: “Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (ishara, dalili) Zetu.” [Al-A’raaf (6: 156)]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾

Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); basi sema: “Rabb wenu ni Mwenye rahmah iliyoenea. Na wala haizuiliwi adhabu Yake kwa watu wahalifu.” [Al-An’aam (6: 147)]

 

 

Rejea pia: Al-A’raaf (7: 56).

 

 

5. Allaah (سبحانه وتعالى) Amewapa fursa makafiri wataraji Rahma na Jannah Yake, lakini ni chaguo lao kukubali haki au kubakia katika upotofu.

 

 

6. Jannah imejaa mazuri yasiyoweza kutambulikana katika akili ya binaadamu. Hadiyth: Al-Qudsiy: ((Nimewatayarishia waja Wangu wema kile ambacho jicho lolote halijapata kuona, na sikio lolote halijapata kusikia, na wala haijapata kupita katika moyo wa binaadamu)). [Al-Bukhaariy na Muslim]  Akasema Abuu Hurayrah: Kwa hivyo, soma ukitaka: ((Basi nafsi yoyote haijui  yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho)). [As-Sajdah (32: 17)]

 

 

7. Moto wa Jahannam na adhabu zake ni kali mno. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

فَالَّذِينَ كَفَرُوا قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ الْحَمِيمُ ﴿١٩﴾

Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto watamwagiwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo.

 

يُصْهَرُ بِهِ مَا فِي بُطُونِهِمْ وَالْجُلُودُ ﴿٢٠﴾

Yatayeyusha kwayo (maji hayo) yaliyomo matumboni mwao na ngozi zao.

 

وَلَهُم مَّقَامِعُ مِنْ حَدِيدٍ ﴿٢١﴾

Na watapata marungu ya vyuma.

 

كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿٢٢﴾

Kila watakapotaka kutoka humo kwa dhiki, watarudishwa humo; na (wataambiwa): “Onjeni adhabu ya kuunguza.” [Al-Hajj (22: 19-22)]

 

 

Rejea pia: An-Nisaa (4: 560, Ibraahiym (14: 15-17), (49-50), Al-Muuminuwn (23: 103-108), Al-Furqaan (25:  65), Asw-Swaaffaat (37: 62-68), Ad-Dukhaan (44: 43-50)  

 

 

  

 

Share