127-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Watakaokuwa Karibu Na Watakaokuwa Mbali Kabisa Na Nabiy Siku Ya Qiyaamah

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

 

Hadiyth Ya 127  

 

Watakaokuwa Karibu Na Watakaokuwa Mbali Kabisa

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  Siku Ya Qiyaamah

 

 

 

 

عَنْ جَابِرٍ ((رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ مِنْ أَحَبِّكُمْ إِلَيَّ وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجْلِسًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ، أَحَاسِنَكُمْ أَخْلاَقًا، وَإِنَّ أَبْغَضَكُمْ إِلَيَّ وَأَبْعَدَكُمْ مِنِّي مَجْلِسًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ، الثَّرْثَارُونَ وَالْمُتَشَدِّقُونَ وَالْمُتَفَيْهِقُونَ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ قَدْ عَلِمْنَا الثَّرْثَارُونَ وَالْمُتَشَدِّقُونَ، فَمَا الْمُتَفَيْهِقُونَ؟ قَالَ: ((الْمُتَكَبِّرُونَ)) رواه الترمذي وَقَالَ حَدِيثٌ حَسَنٌ

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir((رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika wanaopendeza mno kwangu na watakaoketi karibu mno nami Siku ya Qiyaamah, ni wale wenye tabia njema. Na hakika wanaochukiza mno kwangu na watakaokuwa mbali nami Siku ya Qiyaamah, ni wale wenye porojo, wanaojigamba na "mutafayhiquwn")). Wakauliza (Maswahaba): Ee Rasuli wa Allaah! Tumewajua wenye porojo na wanaojigamba. Je, al-mutafayhiquwn ni wepi? Akajibu: ((Ni wenye kiburi)). [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Himizo la kuwa na tabia njema ambayo itamjaalia Muislamu kuwa karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Siku ya Qiyaamah. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amefunza mengi kuhusu tabia njema, kwa kauli na vitendo. Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifu Aliposema:

 وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ﴿٤﴾

Na hakika wewe bila shaka una tabia adhimu. [Al-Qalam (68: 4)]

 

Na Hadiyth ifuatayo inathibitisha:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ الله عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ‏:‏ ((إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ صَالِحَ الأَخْلاقِ‏))

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Hakika nimetumwa ili nikamilishe khulqa (tabia) njema)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy Swahiyh Al-Jaami’ (2349), Swahiyh Adab Al-Mufrad (207)]

 

Rejea pia Hadiyth namba (66).

 

 

2. Makatazo ya kutoa porojo, kwani humpeleka mtu kusema yasiyopasa na yatakayomghadhibisha Allaah (سبحانه وتعالى), au kuudhi watu kwa kila aina za uovu wa ulimi; ghiybah, namiymah, kejeli, istihzai, kuvunja heshima n.k.

 

 

3. Kuzuia ulimi usinene ila yaliyo mema. Allaah (سبحانه وتعالى) Anaonya hayo katika Aayah kadhaa miongoni mwazo ni:

 

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf (50: 18)]

 

 

Pia Hadiyth kadhaa zimeonya kuhusu ulimi na madhara yake.  

 

Rejea Hadiyth namba (86), (87), (88).

 

Rejea pia Al-Israa (17: 36), Al-Hujuraat (49: 11-12), An-Nuwr (24: 15).

 

 

4. Allaah (سبحانه وتعالى) Anatahadharisha kukaa na watu wanaotoa porojo ambao huzifanyia mpaka Aayaat za Allaah (سبحانه وتعالى) porojo.  Anasema  (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾

  Na unapowaona wale wanaoshughulika kupiga porojo katika Aayaat Zetu; basi jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.  [Al-An’aam (6: 68)]

 

Rejea pia: An-Nisaa (4: 140), At-Tawbah (9: 64-66).

 

 

5. Desturi  ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwafunza Maswahaba msimiati isiyozoeleka baina yao katika kuzungumza lugha ya Kiarabu. Lakini hii isifahamike vibaya kwa kuwa Muislamu hapaswi kuzungumza maneno magumu yasiyofahamika khasa ikiwa anaozungumza nao si wenye ujuzi wa lugha anayoizungumza, bali adhihirishe kauli yake ieleweke kwa kutumia maneno ya kawaida. Katazo hili liepushwe katika uandishi pia.

 

 

6 Makatazo ya kujigamba na kuwa na majivuno na kiburi. Allaah (سبحانه وتعالى) Anatahadharisha na Anawachukia wenye kiburi. Anasema:

 

وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿١٨﴾

  “Na wala usiwageuzie watu uso wako kwa kiburi, na wala usitembee katika ardhi kwa maringo, hakika Allaah Hampendi kila mwenye majivuno mwenye kujifakharisha. [Luqmaan (31: 18)]

 

Na pia:

لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿٢٣﴾

Ili msisononeke juu ya yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allaah); na Allaah Hapendi kila mwenye kujinata, anayejifakharisha. [Al-Hadiyd (57: 23)]

 

Rejea pia Hadiyth namba (25), (65).

Share