013-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Uislamu?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

013-Nini Maana Ya Uislamu?

 

 

 

Swali:

 

ما معنى الإسلام

Ni nini maana ya Uislamu?

 

 

 

Jibu:

 

 

ج: معناه الاستسلام لله بالتوحيد والانقياد له بالطاعة والخلوص من الشرك قال الله تعالى (ومن أحسن دينا ممن أسلم وجهه لله) وقال تعالى (ومن يسلم وجهه إلى الله وهو محسن فقد استمسك بالعروة الوثقى)  وقال تعالى  (فإلهكم إله واحد فله أسلموا وبشر المخبتين)

 

Maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumpwekesha na kufuata maamrisho yake kwa utii na kuepukana na shirki kama Allaah (سبحانه وتعالى)  Anavyosema:

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji mazuri na akafuata millah ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki. Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni kipenzi. [An-Nisaa: 125]

 

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

 وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾

Na anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mtenda ihsaan, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni hatima ya mambo yote. [Luqmaan: 22]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ ﴿٣٤﴾

Kwa hiyo Mwabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja Pekee, basi kwake jisalimisheni. Na wabashirie wanyenyekevu. [Al-Hajj: 34] 

 

 

 

Share