Kujikinga Na Shaytwaani Katikati Ya Surah Unaposoma Qur-aan

 

Kujikinga Na Shaytwaan Katikati Ya Suwrah Unaposoma Qur-aan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, ikiwa unasoma Qur-aan na umeanza katikati ya sura inafaa kusema A'udhu BiLLaahi mina-shaytaanir-rajiym

 

 

 

JIBU

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Ni sawa kabisa kuanza kusoma Qur-aan kwa

 

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم

 

 

Ikiwa ni  katikati  ya Suwrah kwani tumeamrishwa kufanya hivyo mtu anapoanza kusoma Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾

Unaposoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa. [An-Nahl: 98]

 

 

Unaweza pia kuongezea na

بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ

 

BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym

 

hata kama ni katikati ya Suwrah.  Na kama ni mwanzo wa Suwrah basi  uanze na

 

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم .   بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ

 

Isipokuwa Suwrah At-Tawbah ambayo inaanzwa kwa 

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم

 

bila ya kusema

بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share