Imaam Al-Albaaniy: Kuhusu Maibaadhi

 

 

Kuhusu Maibadhi

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

 

 

Tutawabainishia kama wako katika uongofu au wako katika upotevu mkubwa. Na bila shaka Maibadhi na kila ambaye anakubaliana na rai yao, na ´Aqiydah yao ya kuwa Maneno ya Allaah (‘Azza wa Jalla) yameumbwa - nayo ni hii Qur-aan Tukufu, na pia anaekataa waumini kumuona Rabb wa walimwengu siku ambayo haitofaa mali wala watoto ila yule aliyekuja kwa Allaah kwa moyo msafi. Bila shaka watu hawa wanaopinga kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah ya kihakika na hayakuumbwa. Kupinga huku kuna upotevu - yaani wa wazi sana.

 

Ama kusema kuwa upotevu huu ni ukafiri na kuritadi kutoka katika dini au hapana, tunasema, ataebainikiwa na hoja (dalili) kisha akakataa huyu ni kafiri karitadi katika dini ya Kiislamu. Lakini mwenye kukataa hilo (kwa ujinga) atakuwa tu katika upotevu. Na sisi si muhimu kusema fulani katika watu au kundi fulani katika watu ni makafiri. Yatosha kusema kuwa ni wapotevu. Kwa kuwa sisi makusudio yetu ni wao waongoke na wajue kuwa wako makosani na kwenye upotevu mpaka warudi katika usawa.

 

Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy

 

 

 

Share