17-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhiyd Ndiyo Inayotenganisha Baina Ya Uislamu Na Ukafiri Au Baina Ya Muislamu Na Kafiri

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

17-Tawhiyd Ndiyo Inayotenganisha Baina Ya Uislamu Na Ukafiri

Au Baina Ya Muislamu Na Kafiri

 

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa waabudiwa badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.” [Aal-‘Imraan: 64]

 

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Na hali hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo. [Al-Maaidah: 73]

 

Neno la Tawhiyd “Laa ilaaha illa Allaah” ndio neno ambalo atakapolitamka mtu akiwa anakiri moyoni kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kumalizia kuamini kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mja na Rasuli wa Allaah, humuingiza katika Uislamu. Lakini Uislamu wake utatimia kikamilifu pale atakapoamini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa Hana mshirika na atakapofuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Vilevile kumwamini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kuamini kwamba hakuna ‘ibaadah au mafunzo yoyote yale isipokuwa aliyokuja nayo yeye Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Muislamu atakapothibitika nalo neno la Tawhiyd, huwa ni ufunguo wake wa Jannah kwa dalili ifuatayo:

 

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :((مَنْ قَالَ: "أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَابْنُ أَمَتِهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَأَنَّ الْجَنَّةَ حَقٌّ وَأَنَّ النَّارَ حَقٌّ" أَدْخَلَهُ اللَّهُ مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةِ شَاءَ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit ambaye amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) amesema: ((Atakayesema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laashariyka lahu, wa anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu – Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake, Hana mshirika na kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah, na ni mwana wa mja wake na Neno Lake Alimtupia Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki” Allaah Atamuingiza Jannah kupitia mlango wowote autakao miongoni mwa milango minane ya Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Abuu Twaalib ambaye ni ‘ammi yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataa kutamka neno la Tawhiyd wakati alipokuwa anafariki, na hivyo juu ya kuwa ni ‘ammi yake ambaye alimhami na maudhi ya makafiri Quraysh wa Makkah, lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemhukumia Moto kwa dalili:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أَهْوَنُ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا أَبُو طَالِبٍ وَهُوَ مُنْتَعِلٌ بِنَعْلَيْنِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ))‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) amesema: ((Adhabu nyepesi kabisa ya watu Motoni ni adhabu ya Abuu Twaalib, atakuwa amevaa viatu [vya moto] vitakavyomsababisha bongo lake kuchemka)).[Muslim]

 

 

Na kisa katika Hadiyth ifuatayo cha kijana wa kiyahudi aliyesilimu:

 

فعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ غُلَامٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعُودُهُ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ فَقَالَ لَهُ: أَسْلِمْ! فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ، فَقَالَ لَهُ أَطِعْ أَبَا الْقَاسِمِ، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ . فَأَسْلَمَ ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَقُولُ : ((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْقَذَهُ مِنْ النَّارِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba kulikuweko na mtoto (kijana mdogo) wa kiyahudi akimhudumia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipoumwa, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kumtembelea, akaketi pembeni ya kichwa chake akamwambia: ((Silimu!)). Mtoto akamtazama baba yake aliyekuweko hapo. Akamwambia: “Mtii Abal-Qaasim Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam”.  Akasilimu. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoka huku akisema: ((AlhamduliLLaah – Himdi ni za Allaah Ambaye Amemuokoa na Moto)). [Al-Bukhaariy (1356), Ahmad (13565) na Abu Daawuwd (3095)]

 

 

Na Tawhiyd ndio sababu ya Al-Walaa wal-Baraa (Kupendana na kuandamana kwa ajili ya Allaah (Dini) na kuchukiana au kutengana kwa ajili ya Allaah)

 

Na ndio maana Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na usuhuba na mapenzi na Bilaal na Maswahaba wengineo waliokuwa watumwa ambao waliingia katika Uislamu kwa sababu ya Dini, na akatengana na Abuu Twaalib na Abuu Lahab kwa sababu ya wao kuikana Dini ya Kiislamu. Hali kadhaalika Maswahaba walitengana na baadhi ya ahli zao kwa sababu ya ukafiri wao. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٢٢﴾

Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao iymaan, na Akawatia nguvu kwa Ruwh (Wahyi) kutoka Kwake, na Atawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.   [Al-Mujaadalah: 22]

 

 

Share