Namna Sahihi Ya Kufungisha Ndoa

SWALI:

 

Wakati wa kufunga ndoa, Walii na muoaji hupeana mikono, Shaykh anayewaozesha anawashikanisha kisha panazungumzwa maneno marefu, je, mheshimiwa Shaykh –Sifa hii (ya ufungishaji ndoa)- imethibiti katika shari’ah?

 


 

JIBU:

 

Kitendo hiki hakina asili, kinachotakikana ni kusoma khutbah ya ndoa: Innal Hamda LiLLaahi…, kisha anaambiwa Walii aseme, ‘nimekuoza bint yangu’ (kama anao wengi atamtaja jina) au ‘nakuozesha dada yangu’,
na ataambiwa muoaji aseme: ‘nimekubali’, basi.
(kuambiana hayo ni mara moja tu hakuna kurudia mara tatu kama ilivyo ada).

Ama kushikanisha mkono wa huyu kwa yule, hili ni jambo ambalo halina asili; ni uzushi usio na dalili yoyote. Bali kinachotakikana kishari’ah ni yule muozeshaji kusoma Khutbah, Innal Hamda liLLaahi nahmaduhu wa nasta’iynuhu… mpaka mwisho, kisha amwambie Walii wa mwanamke, ambaye yeye Walii ni baba yake au kaka yake au mwanae wa kiume au mfano wa hao, amwambie aseme, ‘nimekuozesha ee Fulani kwa Fulani, na muoaji atajibu: ‘nimekubali ndoa hii’. Kisha aseme (muozeshaji): ‘baaraka Allaahu lakumaa’, na awaombee du’aa.

 

Fatwa: Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

smartlives.ws/waheeb/node/6865

Share