Swawm Na Swalah Za Pamoja Ni Bid´ah

 

Swawm Na Swalah Za Pamoja Ni Bid´ah 

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni ipi hukumu ya Swawm ya pamoja (kikundi)?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Ni Bid´ah Swawm ya pamoja ni Bid´ah. Swaalah za pamoja usiku kwa kuambizana hilo watu waamke usiku ili waswali Swaalah ya pamoja... Swaalah ya pamoja na sio Swaalah ya Jamaa´ah, yaani Swaalah ya pamoja, bi maana wewe unaswali kwenye chumba chako, mwingine kwenye chumba chake namna hii. Au wanasimama sehemu moja na kila mmoja anaswali peke yake, hili halijuzu. Hii ni katika Bid´ah iliyozushwa.

 

 

Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

 

 

http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13888

 

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

 

 

 

Share