Watu Wa Matamanio Wanaungana Kwa Uadui Dhidi Ya Watu Wa Haki

 

Watu Wa Matamanio Wanaungana Kwa

Uadui Dhidi Ya Watu Wa Haki

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Imaam Atw-Twabariy (Allaah Amrehemu) amesimulia kuwa Qataadah (Allaah Amrehemu) alisema:

 

 

"Utawakuta watu wa baatwil (upotofu) wakitofautiana wao kwa wao katika ushahidi wao, wakitofautiana katika matamanio yao, na wakitofautiana katika matendo yao. Wakati huo huo, wanaungana kwa uadui wao dhidi ya watu wa haki (wanaofuata msimamo sahihi wa Dini)." [Tafsiyr Atw-Twabariy, mj. 3, uk. 92]

 

 

Haya ni maneno sahihi kabisa na yanaakisi hali iliyopo leo hii. Utakuta makundi yote potofu ya bid'ah na hawaa na itikadi potofu yakiungana kwa uadui dhidi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa'ah (Salafi), japo hayo makundi potofu yenyewe kwa yenyewe hayakubaliani kiundani.

 

 

Kadhaalika, wako vilevile wanaojinasibisha na Sunnah lakini kiundani ni watu wa matamanio, mbali na maadili na akhlaaq, wenye tuhuma, uongo, kuzulia watu na ubinafsi, na wanaozulia uongo na kuwatuhumu Salafi. Wao na wenzao wanaojinasibu kama wao katika Sunnah ilhali wako mbali kabisa na Sunnah kivitendo, kitabia, kimaadili, ki-Manhaj na hata kuifahamu Sunnah yenyewe ilivyo. Huungana wao kwa wao si kwa kupendana, bali kwa kushirikiana katika kuwapiga vita Salafi na kufanya juhudi za kuporomosha kazi na jitihada zao za Da'wah.

 

 

Mtihani huu umeenea katika vyombo vyote vya khabari kama maredio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii na hata kumbi za mawasiliano za kisasa kama whatsapp na zinginezo.

 

 

Na hii ndio changamoto kubwa inayowakabili watu wa haki katika ulimwengu wa Da'wah leo hii.

 

 

Anasema Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah):

 

 

Kama tulivyosema ya kwamba yule atakayefuata Manhaj ya wale walioneemeshwa atapewa mitihani, kupondwa, kudharauliwa, kuonekana kuwa ni mpotevu na kutishwa. Hivyo kunahitajia subira. Ndio maana imekuja katika Hadiyth ya kwamba mtu ambaye anashikama na Dini yake bara bara katika zama za mwisho ni kama mwenye kushika kaa la moto. Hili ni kwa sababu atakutana na maudhi na madhara kutoka kwa watu. Anahitajia kuwa na subira kama mwenye kushika kaa la moto. Hili si kama ngoma kwenye waridi kama wanavyofikiria watu. Hili ndani yake kuna matatizo na maudhi kutoka kwa watu. Linahitajia subira na thabati mpaka ukutane na Rabb Wako na wewe uko katika hali hii ili uokoke na Moto. Utaokoka na upotevu duniani na utaokoka na Moto Aakhirah. Hakuna njia ingine isipokuwa hii.

 

 

 

Leo inapondwa Manhaj ya Salaf kwenye suhuf, magazeti na vitabu. Na wanawaponda vilevile Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Salafiyyuun wa kihakika wanapondwa. Wanasema kuwa wana msimamo mkali na kwamba ni Takfiyriyyuwn (wenye kukufurisha Waislamu) na hivi na vile - lakini hili halidhuru. Lakini linamuathiri yule mtu ambaye hana subira na hana azma yenye nguvu. Hili linaweza kumuathiri.

 

 

Rejea maneno ya Shaykh kwenye kiungo kifuatacho:

 

http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mf04-01-1435.mp3

 

 

 

 

Share