Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan

Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan

 

 

Vipimo - Nyama

Nyama mbuzi - 1 kilo

Kitunguu menya katakata - 1

Nyanya/tungule - 2

Thomu (kitunguu saumu/garlic) saga - 5 chembe

Tangawizi mbichi – kuna/grate au saga - 1 kipande

Pilipili mbichi saga - 2

Bizari ya pilau nzima (cumin seeds) - ½ kikombe cha kahawa

Mdalasini - 1 kijiti

Karafuu nzima - 5 chembe

Gilgilani/dania (coriander seeds) - ½ kikombe cha kahawa

Bizari ya mchuzi - 1 Kijiko cha supi

Chumvi - Kiasi

Mtindi - 1 glass

Hiliki ilopondwa - 2 vijiko vya chai

Vitunguu – menya katakata slices kwa ajili ya kukaanga- 7- 9

Mafuta - Kiasi ya kukaangai vitunguu

 

Vipimo - Wali

Mchele wa pishori/basmati - 4 glass

Zaafarani roweka katika kikombe cha kahawa - Kiasi

Mafuta - Kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Katika sufuria, changanya nyama pamoja, kitunguu kimoja, tangawizi, thomu, nyanya, na viungo vyake isipokuwa mtindi, hiliki na vitunguu vilobakia.


  2. Tia maji kisha funika ichemke mpaka iwive nyama na ikauke supu.


  3. Tia mtindi na hiliki changanya pamoja.


  4. Weka mafuta katika karai, kaanga vitunguu mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Toa uchuje mafuta. Kisha viponde ponde kwa mkono uchanganye na nyama.


  5. Chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji.


  6. Mimina katika nyama utie zaafarani, funika upike wali hadi uwive.


  7. Epua ukiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kufurahika)

 

Share