Wali WaKuku Na Mboga Mchanganyiko

Wali Wa Kuku Na Mboga mchanganyiko

(kutosha kiasi watu 10-15)

 

Vipimo

Mchele wa basmati/pishori - 4 vikombe vikubwa (mugs)

Kuku - 2

Vitnguu vya kijani (sprin onions) katakata - 5 miche

Maharage machanga (spring beans) katakata - kiasi kujaza mug moja

Pilipili boga la (capsicum) katakata - 1

Karoti katakata vipande virefu - 1

Kitunguu thomu (garlic) kuna (grate) - 1 kubwa

Tangawizi mbichi  kuna (grate) - 1 kubwa

Sosi ya soya (soy sauce) - 2 vijiko vya supu

Kidonge cha supu - 1

Mafuta ya kupikia  - ¼ kikombe cha chai

Chumvi - kiasi

Pilipili manga - 1 kijiko cha supu

                                            

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   


  1. Osha kuku vizuri, katakata vipande, weka katika sufuria, tia chumvi, pilipili manga, mfunike, umkaushe motoni huku ukimgeuza geuza.


  2. Roweka mchele kisha uchemshe uive nusu. Chuja maji, tia siagi kidogo ili usigandane.


  3. Weka karai ya kupika mboga (wok) au sufuria kisha tia mafuta yashite moto.


  4. Tia kitunguu thomu, tangawizi, kaanga kidogo.


  5. Tia mboga zote, ulizokatakata.

  1. kaanga kidogo, kisha tia sosi ya soya na kidonge cha supu. Usizipike sana mboga mpaka zikalainika mno. Sababu zitaiva katika mchele

  2. Changanya kuku na mboga kisha changanya vyote katika mchele, urudishe katika moto.


  3. Funika upike hadi uive kamilifu.


  4. Pakua kwenye sahani.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share