007-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-QAYYUWM

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

الْقَيُّوم

 

007 - AL-QAYYUWM

 

 

 

AL-QAYYUWM: Msimamia kila kitu.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Qayyuwm msimamizi wa kila kitu.

Kama ilivyotangulia kutajwa katika Jina la Al-Hayyu kwamba Jina hili limetajwa pamoja na Al-Qayyuwm katika Aayah:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ

Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. [Al-Baqarah: 255 na Aal-‘Imraan: 2]

 

Na:

وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا ﴿١١١﴾

Nyuso zitanyenyekea kwa Aliye Hai daima, Msimamizi wa kila kitu. [Twaahaa: 111]

 

Al-Qayyuwm ni:

1. Mwenye kusimamia mambo Mwenyewe daima. Hakumuhitajia yeyote katika njia yoyote ile kwa sababu ya ukamilifu Wake na kujitosheleza Kwake na uwezo Wake.

 

2. Mwenye kuwasimamia viumbe Vyake, ardhini na mbinguni, wote ni mafakiri Kwake Naye Ndiye tajiri katika kila kitu.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿١٥﴾

Enyi watu!  Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah! Na Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Faatwir: 15]

 

 

Hata ‘Arshi imesimama kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), na wabebaji wake vivyo hivyo.

 

3. Mwenye kusimamia ulimwengu wote, wa juu na wa chini, na waliomo katika viumbe na vitu na katika hali zote: kwa kuwapangia riziki zao, kwa kuwahifadhi na kuwalinda, kuwaongoza katika mambo yote kwa uangalizi na kuwapa kila chenye kuwahitajia wao kubaki kwake, na ustawi wake kila wakati. Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ ﴿٤٩﴾

(Fir’awn) Akasema: “Basi ni nani Rabb wenu ee Muwsaa?”

 

قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾

(Muwsaa) Akasema: “Rabb wetu ni Yule Aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha Akakiongoza.” [Twaahaa: 49-50]

 

Na Anasema:

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ

Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah; na (Allaah) Anajua mahali pake pa kustakiri na pa kuhifadhiwa kwake. [Huwd: 6]

 

4. Yeye Ta’aalaa ni Qayyuwm: Mwenye kusimamia kila kitu, na Mwenye kubaki kuendelea kusimamia kila kitu mpaka baada ya Qiyaamah kuwaingiza waja Wake; Waumini kuingia Jannah na makafiri na waovu kuingi motoni.  Haondoki wala Habadiliki, Anadumu daima kusimaimia kila kitu, Ambaye Hajaacha kuwa na Hatoacha kuwa (kuwepo), Mwenye kusifika kwa ukamilifu na utukufu, katika hali zote: kwa dhati Yake, sifa Zake, matendo yote na utawala Wake.

 

5. Yeye Ndiye Anayeisimamia kila nafsi kwa kuichunga, kuihesabu, malipo kwa kila dogo na kubwa, Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):  

أَفَمَنْ هُوَ قَائِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۗ  

Je, basi Anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma [Ar-Ra’d: 33]

 

6. Usimamizi Wake umekamilika: Amesimamia mbingu na ardhi nazo zimetulia; mbingu zimesimama bila ya kuwa na nguzo, hazitingishiki, mbingu wala haijawahi kuanguka katika ardhi. Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿١٠﴾

(Allaah) Ameumba mbingu bila ya nguzo mnaziona, na Akatupa katika ardhi milima isikuyumbieni yumbieni, na Akaeneza humo kila viumbe vinavyotembea. Na Tukateremsha kutoka mbinguni maji, Tukaotesha humo kila aina ya mimea mizuri yenye manufaa. [Luqmaan: 10]

 

إِنَّ اللَّـهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤١﴾

Hakika Allaah Anazuia mbingu na ardhi zisitoweke. Na zikitoweka, hakuna yeyote wa kuzishikilia baada Yake, hakika Yeye daima Mpole wa kuwavumilia waja, Mwingi wa kughufuria.  [Faatwir: 41]

 

Kisha Siku ya Qiyaamah Atabaidilisha ardhi isiyo ardhi hii na mbingu hali kadhalika.

Na miongoni mwa du'aa za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah za usiku:

اللّهُـمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ  نـورُ السَّمـواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَـيِّمُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ)

Allaahumma Lakal-Hamdu Anta Nuwrus-samaawati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Qayyimus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Rabbus-samawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Laka Mulkus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna....

Ee Allaah! Himdi ni Zako Wewe Ndiye Nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, Himdi ni Zako Wewe Ndiye Msimamizi wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako Wewe Ndiye  Rabb  wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na Himdi ni Zako Wewe Ndiye  Mfalme wa mbingu na ardhi... [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (3/3), (11/116), (13/371, 423, 465), na Muslim kwa ufupi kama hivyo (1/532)]

 

7. Na usimamizi Wake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kupanga Kwake mambo ya viumbe Vyake, na kufanya Kwake mambo kwa ukamilifu na uadilifu na haki, Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ  

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye; na Malaika, na wenye elimu (wameshuhudia kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye [Aal-‘Imraan: 18]

 

8. Na Ukamilifu wa usimamizi Wake ni kwamba Hashikwi na usingizi wala kulala:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ  

Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala  [Al-Baqarah: 255]

 

Na du’aa ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo amesema: baada ya mtu kuomba du’aa hii:

“Kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Tukufu Ambalo Anapoombwa kwalo Anaitikia na Anapotakwa kwalo jambo hutoa:

 اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَـمْدُ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَـريكَ لَـكَ المَنّـانُ يا بَديـعَ السَّمواتِ وَالأَرْضِ يا ذا الجَلالِ وَالإِكْـرام، يا حَـيُّ يا قَـيّومُ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ الجَـنَّةَ وَأَعـوذُ بِـكَ مِنَ الـنّار

Allaahumma inniy as-aluka bi-anna Lakal-Hamdu laa ilaaha illaa Anta Wahdaka laa shariyka Laka Al-Mannaanu yaa Badiy’as-samaawaati wal-ardhwi, yaadhal-Jalaali wal Ikiraami, yaa Hayyu yaa Qayyuwmu, inniy as-alukal-Jannata wa a’uwdhu bika minan-naari

Ee Allaah hakika mimi nakuomba, kwa vile Himdi Zako, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe, Uko Peke Yako,  wala Huna mshirika, Mwingi wa Kuneemesha.  Ee Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Ee Jalali na Mwenye Ukarimu, Ee Uliye hai daima, Msimamizi wa kila kitu, hakika mimi nakuomba Jannah, na najikinga Kwako kutokana na moto.” [Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhiywa Allaahu ‘anhu) - Abu Daawuwd [1495], An-Nasaaiy (3/52), Ibn Maajah [3858] na taz. Swahiyh Ibn Maajah (2/329)]

 

 

 

Share