Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Maana Ya Kuwahama Watu Wa Bid’ah

 

Maana Ya Kuwahama Watu Wa Bid’ah  

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn  (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com  

 

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn  (Rahimahu Allaah) amesema: 

 

“Na muradi wa ‘Kuwahama watu wa bid’ah ni kujiweka mbali nao, na kuacha kuwapenda na kushirikiana nao, na kuwasalimia, na kuwatembelea na kadhaalika.

 

Na kuwahama watu wa bid’ah ni waajib kutokana na kauli ya Allaah (Ta’aalaa):

 

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ   

Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda ambaye anapinzana na Allaah na Rasuli Wake...  [Al-Mujaadalah: 22]

 

na kwa sababu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimhama Ka’ab bin Maalik na wenzake wawili pale walipokhalifu amri ya kwenda vita vya Tabuwk.”

 

 

[Sharh Lum’at Al-I’tiqaad (uk. 110)]

 

 

Share