012-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-BAATWINU

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

الْبَاطِنُ

AL-BAATWINU

 

 

Al-Baatwinu: Aliye karibu kabisa, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾

Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu kabisa hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu kabisa, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.  [Al-Hadiyd: 3]

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

...وَأَنْتَ البَاطِنُ فَليْسَ دُونَكَ شيء...

…Nawe uko karibu kabisa, hakuna kitu kilicho karibu kuliko Wewe...  [Muslim]

 

1. Ibn Jariyr amesema: Naye Ndiye Al-Baatwin kwa vitu vyote, hakuna kitu kilicho karibu zaidi ya kitu kinginecho kuliko ukaribu Wake kama Anavyosema:

وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ ﴿١٦﴾

Na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo. [Qaaf: 16]

 

 

2. Ni wa Ndani, Mwenye kujificha, Asiyeonekana duniani. Mwenye kuweka pazia katika macho ya viumbe, hivyo haonekani duniani. Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana [Al-An’aam: 103]

 

Al-Idraak: Ni kuenea kwa mwenye kudiriki katika kila njia, nayo ni maalum zaidi kuliko kule kuona tu, yeye Ta’ala anaonekana Aakhirah lakini hawezi kuelezewa kwani hakika yake hakudirikiwi na macho. [Tafsiyr Ibn Kathiyr 2/161 na Ibn As-Sa’ady 268.]   

 

 

3-Mwenye kujua mambo ya dhahiri ya ndani, kama vile ambavyo neema Zake nyingi ni za baatwinah (zilizofichika) Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً ۗ وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ ﴿٢٠﴾

Je, hamuoni kwamba Allaah Amekuitishieni vile vilivyomo mbinguni na vile vilivyomo ardhini, na Akakutimizieni kitimilifu neema Zake kwa dhahiri na siri?  [Luqmaan: 20]

 

Mwenye kuangalia na kujua siri za watu, dhamira na yaliyojificha na mambo ya ndani ya siri zake. Hakifichiki chochote au lolote lile la viumbe Vyake katika ‘amali zao za dhahiri wala siri. Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾

Sema: “Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. [Aal-‘Imraan: 29]

Na pia:

يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ ﴿١٩﴾

(Allaah) Anajua khiyana za macho na yale yanayoficha vifua.  [Ghaafir: 19]

 

Kutaabadi kwa jina hili tukufu la Al-Baatwin ni kuabudu kwa mahaba ya kweli, na mapenzi na ya kuwa Allaah kuwa Kwake karibu ya kila kitu pamoja na kuwa Kwake yu dhahiri juu ya kila kitu. [Twariyq Al-Hijratayn 44.]

 

 

Share