Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)

Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)

 

 

Vipimo

Maji baridi – kikombe 1

Biskuti za kawaida – paketi 2

Kaukau (cocoa) – vijiko 3 vya kulia

Kahawa ya unga – kijiko 1 cha kulia

Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa – kikombe 1

Sukari – kiasi upendavyo

  1. Changanya maji na kaukau na kofi na sukari
  2. Katakata biskuti kisha tia paketi moja na nusu uchanganye vizuri.
  3. Kisha nusu ya biskuti zilobakia katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, kisha changanya kidogo tu.
  4. Weka katika foil paper na zungusha (roll)
  5. Kisha fungua umwagie njugu au mkassaraat zilosagwa
  6. Kisha roll katika foil paper na uweke katika freezer mpaka igande
  7. Kisha kata kata slices na iko tayari

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

Share