Kufanya Kazi Ya Kufunga Magari Barabarani Inafaa?

 

SWALI:

Assalam Alaykum.

napenda kuuliza tu Kazi ya kufunga magari barabarani inafaa.

Yaani (Clamp) kazi hii unaajiriwa kwa kuklamp magari yaliyopaki sehemu iliyokua hairuhusiwi

Swali ni kazi ya clamp ifaa.

Waasalam Alaykum


 

 

JIBU:

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kazi hiyo haina ubaya kufanya, kwani bila shaka itakuwa ni makosa ya mwenye kuweka gari lake katika sehemu isiyoruhusiwa, na bila ya shaka kutakuwa kumewekwa tangazo au alama kuwa sehemu hiyo haifai kuwekwa magari. Na mara nyingi huwekwa maelezo bayana kwa kutajwa kama pindi mtu akiweka gari lake basi itakuwa ni juu ya mtu binafsi litakalotokea.  Matokeo yake ni kuchukuliwa kwa kuvutwa na itakuwa ni jukumu lake mwenyewe aliyeweka gari ovyo. Na wewe  umeajiriwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo basi ni wajibu wako kutekeleza.

Vile vile ni wajibu wa wananchi kutimiza na kufuata sheria za serikali kwa sababu, sheria kama hizo ni kwa ajili ya  usalama, amani, himaya, usafi  na kuepusha msongamano wa magari barabarani katika mji huo anaoishi mtu.  

Kwa hivyo hatuoni kama una ubaya wowote kufanya kazi kama hiyo.

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share