09-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

09-Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?

 

Faida ya Tawhiyd kwa Muislamu ni kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani  Aakhirah.

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka. [Al-An’aam: 82]

 

((وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلى اللهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) متّفق عَلَيهِ

((Haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote kile)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share