14-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Ni yapi madhara ya kumshirikisha Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

14-Ni yapi madhara ya kumshirikisha Allaah?

 

Madhara ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) husababisha kudumu milele motoni.

 

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ

Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni.  [Al-Maaidah: 72]

 

((من ماتَ يُشرِك باللهِ شيئاً دخل النّار))   رواه مسلم

((Atakayekufa na huku amemshirikisha Allaah kwa chochote, ataingia motoni)) [Muslim]

 

 

 

 

 

 

Share