17-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukumu ya kumuomba asiye Allaah kama Mawalii?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

17-Nini hukumu ya kumuomba asiye Allaah kama Mawalii?

 

 

Hukmu ya kuwaomba ‘Mawalii’ ni shirki yenye kumpeleka mtu motoni.

 

فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ ﴿٢١٣﴾

Basi usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa. [Ash-Shu’araa: 213]

 

((من ماتَ وَهُوَ يدعو مِن دون الله نِدّاً دخل النّار)) رواه البخاري

((Atakayefariki katika hali ya kumuomba asiye Allaah ataingia motoni)) [Al-Bukhaariy]

 

 

Mawalii:  Waliokusudiwa hapa ni watu wema waliofariki wakaombwa wao makubirini badala ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au wakatumiliwa kama ni tawassul ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). 

 

 

 

 

Share