37-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Unahitaji kumuomba Allaah kumtegemea kiumbe yeyote?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

37-Je, Unahitaji kumuomba Allaah kumtegemea kiumbe yeyote?

 

Hapana! Huhitaji kumtegemea kiumbe mwengine unapomuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ

Na watakapokuuliza waja Wangu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.  [Al-Baqarah: 186]

 

((إِنَّكُمْ تَدْعُونَ سَمِيعًا قَرِيبًا وَهُوَ مَعَكُمْ))  رواه مسلم

((Hakika nyinyi mnamuomba Mwenye kusikia, Aliye karibu (nanyi) Naye Yuko na pamoja nanyi [kwa ujuzi Wake])) [Muslim]

 

 

 

Share