50-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je? Tunaweza kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah Na Rasuli Wake?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

50-Je? Tunaweza kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah Na Rasuli Wake?

 

 

Hapana! Haifai kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Yaani: Msilete rai zenu wala msifanye kinyume na Aliyoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾

Enyi walioamini! Msikadimishe (lolote) mbele ya Allaah na Rasuli Wake [Al-Hujuraat: 1]

 

((لَا طَاعَة لأحدَ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ)) متّفق عَلَيهِ

((Hakuna kumtii mtu yeyote katika kumuasi Allaah, Bali Utiifu ni katika mambo mema)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share