60-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Nabiy ‘Iysaa atateremka duniani kuwa ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

60-Je, Nabiy ‘Iysaa atateremka duniani kuwa ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah?

 

Naam! Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) atateremka kutoka mbinguni kuja duniani kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah.

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا﴿١٥٩﴾

Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao [An-Nisaa: 159]

 

((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا)) 

((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share