04-Kitaab At-Tawhiyd: Kukhofia Shirki

Mlango Wa 4

بَابُ الْخَوْفِ مِنْ اَلشِّرْكِ

Kukhofia Shirki

 


 

وَقَوْلِ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ:

Na kauli Yake ‘Azza wa Jalla:  

 إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

((Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae)) [An-Nisaa (4: 48, 116)]

 

وَقَالَ الْخَلِيلُ عَلَيْهِ اَلسَّلامُ :

Na amesema Khaliyl (Ibraahiym  (عليه السلام

 وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ ﴿٣٥﴾

((na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu)) [Ibraahiym (14: 35)]

 

وَفِي الْحَدِيثِ: ((أَخْوَفُ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمْ اَلشِّرْكُ الأَصْغَرُ)) فَسُئِلَ عَنْهُ فَقَالَ:  ((اَلرِّيَاءُ))

Na katika Hadiyth: ((Nnachokukhofieni zaidi juu yenu ni shirki ndogo)) Akaulizwa kuhusu hiyo shirki akasema: ((Riyaa)) [Ahmad katika Musnad yake (429, 428/5)]

 

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اَللَّهِ نِدًّا دَخَلَ اَلنَّارَ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ.

Na Imepokelewa kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Yeyote atakayekufa hali anamshirikisha Allaah ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy]

 

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((مَنْ لَقِيَ اَللَّهَ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا, دَخَلَ الْجَنَّةَ. وَمَنْ لَقِيَهُ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا; دَخَلَ اَلنَّارَ))

Na kwa Muslim Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه)   kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayekutana na Allaah hali hamshirikishi na chochote ataingia Jannah. Na atakayekutana Naye hali anamshirikisha na chochote ataingia motoni)) [Muslim (93)]

 

 Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kukhofia shirki.

 

2-Riyaa ni aina ya shirki.

 

3-Riyaa ni shirki ndogo.

 

4-Riyaa inakhofiwa sana na waja wema (kwani rahisi mno mtu kutumbukia ndani yake)

 

5-Ukaribu wa Jannah na moto.

 

6-Ukaribu huo wa Jannah na Moto umetajwa katika Hadiyth moja.

 

7-Mwenye kukutana na Allaah (Siku ya Qiyaamah) akiwa hakumshirikisha na chochote ataingia Jannah; na mwenye kukutana Naye, huku amemshirikisha na kitu, ataingia motoni, hata kama alikuwa ni miongoni mwa wanaomwabudu mno Allaah (سبحانه وتعالى).

 

8-Umuhimu mkubwa mno wa suala hili, kiasi kwamba Al-Khaliyll (Ibraahiym) aliomba yeye na wanawe waepushwe dhidi ya kuabudu masanamu.

 

9-Kuzingatia kwake jinsi watu wengi walivyoingia katika ibaadah ya masanamu pindi aliposema:

 

رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ

((“Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza wengi sana katika watu)) [Ibraahiym (14:36)]

 

10-Tafsiri ya maana ya (kauli ya) “Laa ilaaha illaa Allaah” kama alivyoitaja Al-Bukhaariy.

 

11-Fadhila za aliyesalimika na shirki.

 

 

 

 

Share