06-Kitaab At-Tawhiyd: Tafsiri Ya Tawhiyd Na Shahaadah: Laa Ilaaha Illa-Allaah

 

Mlango Wa 6

بَابُ تَفْسِيرِ التَّوْحِيدِ وَشَهَادَةِ أنْ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ

Tafsiri Ya Tawhiyd Na Shahaadah: Laa Ilaaha Illa-Allaah


 

وَقَوْلِ اللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾

((Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako daima ni ya kutahadhariwa)) [Al-Israa (17: 57)]

 

وَقَوْلِهِ:  

Na kauli Yake:

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ ﴿٢٦﴾

((Na Ibraahiym alipomwambia baba yake na kaumu yake: “Hakika mimi nimejitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu.

 

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ ﴿٢٧﴾

 ((“Isipokuwa Ambaye Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoza.”))

 

وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢٨﴾

((Na akalifanya neno (laa ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea)) [Az-Zukhruf (43: 26-28)]

 

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٣١﴾

((Wamewafanya wanachuoni wao mafuqahaa wa dini na Wamonaki wao kuwa ni miola badala ya Allaah, na (pia wamemfanya) Al-Masiyh mwana wa Maryam (kuwa ni muabudiwa); na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah (Allaah) Mmoja Pekee. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Subhaanah! Utakasifu ni Wake! kutokana na yale yote wanayomshirkisha nayo)) [At-Tawbah (9: 31)]

 

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

((Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wangelitambua wale waliodhulumu watakapoona adhabu kwamba nguvu zote ni za Allaah; na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu)) [Al-Baqarah (2: 165)]

 

وفِي الصَّحِيحِ عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أنَّهُ قَالَ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ، وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللَّهِ؛ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ، وَحِسَابُهُ عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ))

Na katika Swahiyh Muslim, kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mwenye kusema: laa ilaaha illa-Allaah, na akakanusha yote yanayoabudiwa pasina Allaah, basi imeharamishwa mali yake [kufanywa ghanima n.k.] na damu yake na hisabu yake itakuwa kwa Allaah ‘Azza wa Jalla)) [Muslim (23) Ahmad (472/3]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Mlango huu umetaja jambo kubwa na muhimu kabisa nalo ni maelezo ya Tawhiyd na Shahaadah na kubainishwa kwake kwa mambo ya dhahiri.

 

2-Mojawapo ni Aayah ya Suwratul-Israa, ni ukanusho wa dhahiri dhidi ya washirikina wanaoomba waja wema na pia kubainisha kwamba kufanya hivyo ni shirki kubwa.

 

3-Pia Aayah ya Suratul-Baraa (At-Tawbah) imebainisha wazi kwamba Ahlul-Kitaab waliwafanya Wanachuoni wao na watawa kuwa ni waabudiwa badala ya Allaah (سبحانه وتعالى). Pia ni dhahiri kwamba hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah Mmmoja; Allaah (سبحانه وتعالى). Tafsiri ya Aayah haina utata kuhusu utiifu wao kwa Wanachuoni na waja wengine wa Allaah (سبحانه وتعالى) katika yasiyo maasi; (yaani inajuzu kuwatii katika yanayaokubalika kishariy’ah), lakini haijuzu kuwaomba (du’aa) au kuwaabudu.

 

4-Pia kauli ya Ibraahiym (عليه السلام) kwa makafiri,

إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ ﴿٢٦﴾

((“Hakika mimi nimejitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu)).

 

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي

((“Isipokuwa Ambaye Ameniumba...”)).

 

Kauli yake hiyo Ibraahiym (عليه السلام) inatutambulisha kwamba amejitoa dhima (kwa kujjiweka mbali) na shirki kwa kuwa amekataa kumuabudu yeyote asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Pia inathibitisha Shahada ya Laa ilaaha illa-Allaah kwani Anasema:

 

وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢٨﴾

((Na akalifanya neno (laa ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea)).

 

5-Kuna Aayah katika Suwratul-Baqarah kuhusu makafiri ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ ﴿١٦٧﴾

((wala hawatokuwa wenye kutoka motoni)) [Al-Baqarah (2: 167)]

 

Imetajwa kwamba wanawapenda wanaowashirikisha na Allaah (سبحانه وتعالى) kama wanavyompenda Allaah. Na hii inathibitisha kwamba mapenzi yao juu ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni makubwa, lakini hivyo haikuwaingiza katika Uislamu. Itakuwaje basi hali ya anayempenda muabudiwa wa uongo kuliko kumpenda Allaah? Na itakuwaje basi aliyekuwa hapendi yeyote isipokuwa muabudiwa wa uongo na wala hana mapenzi na Allaah?

 

 

6-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ، وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُون اللَّهِ؛ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ، وَحِسَابُهُ عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ

((Mwenye kusema: laa ilaaha illa-Allaah, na akakanusha yote yanayoabudiwa pasina Allaah, basi imeharamishwa mali yake [kufanywa ghanima n.k.] na damu yake na hisabu yake itakuwa kwa Allaah ‘Azza wa Jalla))

 

Hii ni kauli nzito kabisa ya kufafanua maana ya laa ilaaha illa-Allaah. Inadhihirisha kwamba kuitamka tu hailindi damu na mali ya mtu. Wala haitoshelezi kufahamu maana yake au kuikiri, au hata awe hamuombi mwengine isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee; bali mali na damu ya mtamkaji haiharamishwi mpaka juu ya hayo iweko nyongeza ya kwamba, akanushe kabisa kila kinachoabudiwa asiyekuwa Allaah. Na akitilia shaka au akiwa anasitasita, basi mali na damu yake haitokuwa ni haramu (haitokuwa katika ulinzi na amani). Basi mfano gani zaidi ya huu utatolewa? Kipi kitakachofafanua nukta hii waziwazi?  (Hakika) Ina hoja nzito inayokata mzozo (wa kuhusu maana ya laa ilaaha illa-Allaah)

 

 

 

 

 

 

 

 

Share