15-Kitaab At-Tawhiyd: Kinachoombwa Haiwezekani Kuwa Kiabudiwe

Mlango Wa 15

باب: أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ

Kinachoombwa Haiwezekani Kuwa Kiabudiwe


 

قَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Kauli ya Allaah Ta’aalaa:

أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ ﴿١٩١﴾

((Je, wanawashirikisha (na Allaah) wale ambao hawaumbi kitu na hali wao wameumbwa?))

 

وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٢﴾

((Na wala hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao)) [Al-A’raaf (7: 191-192]

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake: 

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

((Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende))

 

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾

((Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatokuitikieni. Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kama Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika)) [Faatwir (35: 13-14)]

 

في الصحيح عن أنس (رضي الله عنه)  قال: شُجَّ النبيُّ  (صلى الله عليه وسلم) يوم أُحُدٍ وكُسِرَتْ ربَاعِيَتُهُ، فقال: ((كيف يُفْلِحُ قومٌ شَجُّوا نبيَّهم)) فنزلت: ((لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ))

 

Katika Swahiyh imepokelewa kutoka kwa Anas(رضي الله عنه)  amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alijeruhiwa Siku ya vita vya Uhud meno yake yakavunjika. Akasema: ((Watafaulu vipi watu wanaomjeruhi Nabii wao)) Ikateremka Aayah: ((Si juu yako katika jambo hili)) [Aal-‘Imraan (2: 128)]

 

وفيه عن ابْنِ عُمَر (رضي الله عنهما) أَنه سَمعَ رسول الله  (صلى الله عليه وسلم) إِذا رَفَعَ رأسَه من الرُّكُوعِ فِي الرَّكْعَةِ الأخِيرَة مِنَ الْفَجْرِ: ((اللَّهم العَنْ فُلاَناً وَفُلانًا)) بعدما يقول: سَمِعَ اللّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَبَّنا وَلَكَ الْحَمْد فأنزل الله: ((لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ))

وفي رواية: يَدْعو على صَفوانَ بن أُميَّة وسُهَيْلِ بن عَمرو والحارثِ بن هِشَام. فنزلت: ((لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ))

Imenukuliwa humo pia kutoka kwa Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) amemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa baada ya kurukuu katika rakaa ya mwisho kwenye Swalaah ya Alfajiri: ((Allaahumma mlaani fulani na fulani)) Allaah Akateremsha:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu”   Aal-‘Imraan (2: 128)].

 

Na katika riwaayah: Akiwaapiza Swafwaan bin Umayyah, Suhayl bin ‘Amr na Al-Haarith bin Hishaam, ikateremka:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu”    [Aal-‘Imraan (2: 128)].

 

وفيه عن أبي هُريرةَ (رضىِ الله عنه) قال: قام رسوِل الله  (صلى الله عليه وسلم) حين أُنزل عليه ((وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ )) فقال: ((يا مَعْشَرَ قُرَيش!)) - أو كلمة نحوها: ((اشتَرُوا أنفُسَكُم، لا أُغْنِي عَنْكُم مِنَ الله شيئاً، ويا عبَّاسُ بن عَبْدِ المُطَّلِبِ لا أُغْنِي عَنْكَ مِنَ الله شيئاً، وَيا صَفِيَّةُ عَمَّةَ رسولِ الله، لا أُغْنِى عَنْكِ مِن الله شيئاً، ويا فَاطِمَةُ بِنْتَ مُحمدٍ سَلِينِي مِنْ مَالِي مَا شِئْتِ، لا أُغْنِي عَنْكِ مِنَ الله شيئاً))

Imenukuliwa humo pia kutoka Abuu Hurayrah (رضىِ الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama ilipoteremshwa

 

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ

((Na onya jamaa zako wa karibu)) [Ash-Shu’araa (26: 214)].

 

Akasema: ((Enyi hadhara ya Quraysh)) - au maneno kama hayo - ((Okoeni nafsi zenu, kwani sitowafaeni kwa chochote mbele ya Allaah!  Ee ‘Abbaas bin ‘Abdil-Muttwalib! Sitokufaa kwa chochote mbele ya Allaah!  Ee Swafiyyah shangazi yake Rasuli wa Allaah! Sitokufaa kwa chochote mbele ya Allaah! Ee Faatwimah bint Muhammad! Niombe mali utakayo, [lakini] sitokufaa kwa chochote mbele ya Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri za Aayah: (Al-Araaf 7: 191-192 na Faatwir 35: 13-14).

 

2-Kisa cha Uhud.

 

3-Qunuwt (du’aa) ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalaah ikiitikiwa Aamiyn na Maswahaba nyuma yake.

 

4-Wale walioombewa dhidi yao du’aa, ni miongoni mwa makafiri.

 

5-Maquraysh walifanya mambo ambayo makafiri wengi hawakuyafanya, walimpiga Nabiy wao na kumjeruhi kichwani na kuazimia kumuua, kuikatakata miili ya Waislamu waliouawa japokuwa walikuwa ni banu ‘Ammi zao.  

 

6-Juuu ya hivyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Alimpelekea Wahyi kuhusu hilo:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ 

 

Jambo hili halikuhusu wewe; 

 

7-Baada ya Wahyi kuhusu kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى):

أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ

((ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu)) [Aal-‘Imraan (2:128)].

 

Akawapokelea tawbah na wakaamini.

 

8-Qunuwt inajuzu wakati wa majanga.

 

9-Kuwataja wanaoapizwa du’aa katika Swalaah kwa majina yao na ya baba zao.

 

10-Kulmlaani mtu wakati wa Qunuwt.

 

11-Kisa na hali ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati alipotumiwa Wahyi wa Aayah:

 

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾

((Na onya jamaa zako wa karibu)) [Ash-Shu’araa (26: 214)]

 

12-Uzito wa jambo hili kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (alifanya bidii kutekeleza da’wah hadi) kufikia kuitwa mwendawazimu na ndivyo hali itakavyokuwa kwa Muislamu yeyote atakapofanya hivyo leo. 

 

13-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwatangazia nduguze wote wa karibu na wa mbali: ((Sitowafaeni chochote mbele ya Allaah!)) Hata alisema: ((Ee Faatwimah bint Muhammad, sitokufaa kwa chochote mbele ya Allaah)).

 

Ikiwa yeye ni Sayyid wa Manabii na kaliweka wazi hilo, kwamba hatoweza kumfaa chochote mbora wa wanawake duniani (binti yake Faatwimah) na mtu akaamini kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hasemi ila haki, kisha tazama yanayotokeza katika nyoyo za watu leo (kupendelea jamaa zao), hapo itadhihirika kwako suala la Tawhiyd na maajabu ya Dini![1]

 

 

[1] Kuhusu Hadiyth iliyosimuliwa na Muslim ((Hakika umekuja uislamu katika ugeni na utarejea tena katika ugeni na bishara njema kwa watakaokuwa wageni [watendaji watanufaika na mti wa Jannah]).

Share