21-Kitaab At-Tawhiyd: Kutukuza Mno Makaburi Ya Waja Wema Huyafanya Masanamu Yaabudiwayo

Mlango Wa 21

بَابُ مَا جَاءَ أَنَّ الْغُلُوَّ فِي قُبُورِ اَلصَّالِحِينَ يُصَيِّرُهَا أَوْثَانًا تُعْبَدُ مِنْ دُونِ اَللَّهِ

Kutukuza Mno Makaburi Ya Waja Wema Huyafanya

Kama Masanamu Yaabudiwayo Badala Ya Allaah


 

 

رَوَى مَالِكٌ فِي الْمُوَطَّأِ: أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((اَللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْ قَبْرِي وَثَنًا يُعْبَدُ اِشْتَدَّ غَضَبُ اَللَّهِ عَلَى قَوْمٍ اِتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ))  

Amepokea Imaam Maalik katika Al-Muwattwaa kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ee Allaah! Usijaalie kaburi langu kuwa sanamu la kuabudiwa. Ghadhabu za Allaah zimezidi kwa watu wanaofanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti)) [Maalik fiyl Muwattwaa]

 

وَلاِبْنِ جَرِيرٍ بِسَنَدِهِ عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ: ((أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ)) قال: كَانَ يَلُتُّ لَهُمْ اَلسَّوِيقَ،  فَمَاتَ، فَعَكَفُوا عَلَى قَبْرِهِ

Ibn Jariyr (Atw-Twabariy) kwa isnaad yake, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Mujaahid kuhusu Aayah: ((Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa?)) [An-Najm (53: 19)] Amesema: “(Laata) Alikuwa akiwahudumia mahujaji sawiyq.[1] Baada ya kufa kwake, watu wakaanza kusabilia kaburi kwa ‘ibaadah.” 

 

وَكَذَا قَالَ أَبُو الْجَوْزَاءِ عَنْ اِبْنِ عَبَّاس:  كَانَ يَلُتُّ اَلسَّوِيقَ لِلْحَاجِّ.

Na Hadiyth hiyo imesimuliwa na Abu Al-Jawzaai kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema pia: “Alikuwa akiwakaribisha sawiyq kwa mahujaji.”

 

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) قَالَ: لَعَنَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) زَائِرَاتِ الْقُبُورِ، وَالْمُتَّخِذِينَ عَلَيْهَا الْمَسَاجِدَ وَالسُّرُجَ. رَوَاهُ أَهْلُ اَلسُّنَنِ

Imepokelewa toka kwa Ibn Abbaas(رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا)  amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewalaani wanawake wanaozuru makaburi, na wanaojenga Misikiti kwenye makaburi na kuyawashia taa makaburi” [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Ufafanuzi kuhusu ‘awthaan’ (masanamu).

 

2-Ufafanuzi kuhusu ‘ibaadah.

 

3-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuomba kinga kwa Allaah (سبحانه وتعالى) isipokuwa kwa alichokhofia kutokea.

 

4-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuambatanisha kwake du’aa: ((Ee Allaah! Usijaalie kaburi langu…)) pamoja na (kukhofia khatari ya) ((watu wanaofanya makaburi ya Manabii kuwa Misikiti)).

 

5-Kutajwa ghadhabu kali za Allaah (kwa anayefanya kitendo hicho).

 

6-La muhimu kabisa ni maelezo kuhusu ‘ibaadah ya Laata ilivyoanza, nalo ni sanamu kuu kabisa kabla ya Uislamu.

 

7-Asili ya Laata lilikuwa ni kaburi la mja mwema.

 

8-Laata ni jina la mtu aliyezikwa katika kaburi hilo na ndio maana sanamu hilo likaitwa hivyo.

 

9-Laana (ya Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم ) kwa wanawake wanozuru makaburi. 

 

10-Laana ya Nabiy kwa wanaoweka taa kwenye makaburi.

 

[1] Mikate kutokana na unga wa shayiri uliochanganywa na maji na samli.

 

 

 

Share